FADIHLA YA KUDUMU KATIKA TAUHIDI (KUMPOKESHA MWENYEZI MUNGU)


5847
wasifu
Umoja wa Mwenyezimngu ndio msingi mkubwa ambao zimesimama juu yake mbingu na ardhi, na kwa ajili yake waliuimbwa binadamu na majini na wametumilizwa Mitume. Na kwa kadiri ya mtu anvyompwekesha Mwenyezi Mungu na kumtakasia, na anavyojiepusha na ushirikina wa nje na wa ndani ndivyo kadiri anavyokuwa katika amani na uongofu wa duniani na Akhera

Utangulizi

Shukrani za dhati ni kwa Mola Mkarimu. Rehma na amani zimfikie Mtume Muhammad. Tutazungumzia katika khutba hii mambo yafuatayo:- kubainisha umuhimu wa Tawhidi na fadhila zake, kubainisha kwamba Tawhidi ni sababu ya kuokoka mwanadamu siku ya kiama na pia kubainisha kwamba Tawhidi ni sababu ya kuondoshewa balaa na fitna vile vile nibainishe umuhimu mkubwa wa kujifundisha Tawhidi na shirki kwa aina zake.

Ama baada ya haya, Tawhidi ni msingi mkubwa ambao Mwenyezi Mungu amewaumba majini na watu kwa ajili yake. Kwani Mwenyezi Mungu hakuwaumba majini na watu isipokuwa kwa kumuabudu yeye.

(وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنْسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ ) [الذاريات: 56]

Amesema Mola (Subhaanahu wa Taala) : {{Sikuwaumba majini na watu isipokuwa waniabudu}} [Addhariyati : 56].

Ndugu katika imani na wausia kumcha Mwenyezi Mungu kwa siri na kwa dhahiri na jueni ya kwamba moyo wa Muislamu hauwi mzuri isipokuwa kwa Tawhidi. Kwani Tawhidi ni jambo kubwa. Allah (Subhaanahu wa Taala) Amelibainisha katika kitabu chake na pia Mtume, rehma na amani zimfikie ameliweka wazi katika hadithi zake tukufu.Tawhidi ni jambo ambalo hawezi kuokoka mtu yoyote duniani na kesho Akhera ila alikamilishe jambo hilo la kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kutomshirikisha na chochote. Amesema Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam): [Atakaye kufa na akijua ya kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu ataingia peponi].

Umuhimu wa Tawhidi

Tawhidi ni jambo bora sana, na kwa sababu hii Allah (Subhaanahu wa Taala) Ameshuhudia kwa nafsi yake vile vile Malaika wameshuhudia na pia waliopewa ilimu. Na hii ni kuonesha ubora wa jambo hili la Tawhidi. Jambo Amelishuhudilia Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala), wakashuhudia Malaika watukufu na pia wanadamu watukufu na watu waliopewa ilimu.

(شَهِدَ اللَّهُ أَنَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ) [آل عمران: 18]

Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala): {{Ameshuhudia Mwenyezi Mungu ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa yeye na Malaika na pia waliopewa ilimu,hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa yeye Mwenye nguvu Mwenye hekima}} [Al-Imran : 18 ].

Miongoni mwa umuhimu wa Tawhidi ni kwamba Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) Alilingania Tawhidi kuanzia mwanzo wa ulinganizi wake hadi mwisho wa uhai wake, bali Mitume wote walilingania hivyo.

Pia tunapata katika sira ya Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) ya kwamba alipokuwa akituma maswahaba kwenda kulingania katika sehemu fulani huwausia kwanza kuwalingania Tawhidi.

Miongoni mwa umuhimu wa Tawhidi ni kwamba mwenye kushikamana na Tawhidi husamehewa dhambi zake na anaepushwa kukaa motoni.

Mwenye kushikamana na Tawhidi huwa karibu zaidi na Mwenyezi Mungu na pia hupata amani kamili na uongofu hapa duniani na kesho akhera.

قال تعالى) : الَّذِينَ آَمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُمْ بِظُلْمٍ أُولَئِكَ لَهُمُ الْأَمْنُ وَهُمْ مُهْتَدُونَ) [الأنعام: 82]

Amesema Mola (Subhaanahu wa Taala): {{Wale walioamini na wasichangane imani zao na dhulma watapata amani na wataongoka}} [Al-Anaam : 82]. Kwa mujibu wa Aya hii ni kwamba Muislamu anayeshikamana na Tawhidi atakuwa na amani hababaiki hapa duniani yuwajua litakalompata hapa duniani ni kadari ya Mola (Subhaanahu wa Taala) na kuwa atapata amani kesho akhera.

Bila ya kusahau kuwa endapo waumini watashikamana na tauhudi wataondoshewa balaa na fitna kesho akhera. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Anayeshuhudia ya kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa yeye asiyekuwa na mshirika na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na kwamba Nabii Isa ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na neno lake alilolitia kwa Mariam na roho kutoka kwake na pepo ni haki na moto ni haki Mwenyezi Mungu atamwingiza peponi kulingana na amali].

Ni vyema niwatajie mifano ya ambao waliepushiwa balaa na fitna.Tutoe mfano katika Mitume walioepushiwa balaa na fitna ni Nabii Ibrahiim pale walipokuwa watu wake wanataka kumchoma Mwenyezi Mungu Alimwokoa kwa kuuambia moto: “Ewe moto kuwa baridi na salama kwa Ibrahim” na ikawa kama alivyotaka Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Na Mtume mwengine ni Nabii Lut pale Mwenyezi Mungu Alipowaangamiza watu wake na kumwokoa yeye na waliomwamini yeye na mifano ya walioepushiwa balaa na fitna ni mingi na sababu ya kuepushiwa balaa ni kwa sababu ya kushikamana kwao na Tawhidi. Enyi waumin! Napenda kutaja bali kufafanua japokuwa kwa uchache aina za Tawhidi.

Aina ya Tawhidi:

Tawhidi ya vitendo vya Mwenyezi Mungu nayo ni kumpwekesha Yeye katika uumbaji na uendeshaji wa mambo ya viumbe, na hashirikiani na yoyote katika hilo yoyote.

قال تعالى) : اللَّهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَأَنْزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَكُمْ وَسَخَّرَ لَكُمُ الْفُلْكَ لِتَجْرِيَ فِي الْبَحْرِ بِأَمْرِهِ وَسَخَّرَ لَكُمُ الْأَنْهَارَ) [إبراهيم: 32]

Amesema Mola (Subhaanahu wa Taala): {{Mwenyezi Mungu ndiye aliyeumba mbingu na ardhi na ameteresha kutoka mawinguni maji akatoa kwa maji hayo mazao hali yakuwa ni riziki kweni nyinyi na akawadhalilishia majahazi ili yapite katika bahari kwa amri yake, na akawadhalilishia nyinyi mito ya maji} [Ibrahim: 32 ].

Tawhidi aina ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika ibada. Maana ya maneno haya ni kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Anayefaa kuabudiwa.

قال تعالى) : إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ) [الفاتحة: 5]

Asema Mola (Subhaanahu wa Taala): {{Ni wewe tu tunakuabudu na kwako wewe peke yako tunataka msaada}} [Al-Faatiha : 5].

Tawhidi ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika Sifa Zake na majina yake. Maana yake ni kwamba Mwenyezi Mungu hafanani na yoyote katika Sifa Zake na majina.Wala hafai yoyote kujifananisha wala kumfananisha yoyote na Mwenyezi Mungu katika sifa au majina yake kwani hana mfano wa yoyote.

قال تعالى) : قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ 1اللَّهُ الصَّمَدُ 2لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ 3وَلَمْ يَكُنْ لَهُ كُفُوًا أَحَدٌ 4) [الإخلاص1: 4]

Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala): {{Sema; Mwenyezi Mungu ni mmoja Mwenyezi Mungu Ndiye Anayetakwa msaada, hakuzaa wala hakuzaliwa na Hana mfano Wake yoyote}} [Al-Ikhlas 1 - 4].

Aina zote za Tawhidi ni lazima kwa Muislamu azijue na azitumie katika maisha yake na hii ni kwa faida ya Muislamu. Na endapo mtu ataenda kinyume na aina hizi za Tawhidi basi ameshajitia matatizo duniani na kesho akhera, kwani Mwenyezi Mungu hamsamehe anayekufa katika shirki bila yakutubai.

قال تعالى) : إِنَّ اللَّهَ لَا يَغْفِرُ أَنْ يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَلِكَ لِمَنْ يَشَاءُ وَمَنْ يُشْرِكْ بِاللَّهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا) [النساء: 116]

.

Amesema Mola (Subhaanahu wa Taala): {{Hakika Mwenyezi Mungu hamsamehe anayemshirikisha na Anamsamehe isiyokuwa shirki kwa anayemtaka}} [An-Nisaa : 116].

Enyi ndugu katika imani!Napenda kuchukua fursa hii kutaja mambo ambayo yanakwenda kinyume na Tawhidi. Mambo ambayo anatakiwa Muislamu ayajue na ajiepushe nayo baada ya kuyajua. Mshairi amesema:»Nimeijua shari si kwa ajili ya kuifanya, lakini kwa ajili ya kuiepuka na asiyejua kheri kutokamana na shari ataingia katika shari hiyo.»

Mambo yanayo Haribu Tawhidi

Miongoni mwa mambo ambayo yanatakiwa ajitahadhari nayo yasije yakamtia katika matatizo dunaini na siku ya kiama. Miongoni mwa mambo hayo:-

- Ushirikina kwa aina zake zote. Kwani shirki kubwa inafutilia mbali imani. Na shirki ndogo ina punguza ukamilifu wa Tawhidi.Na mfano wa shirki ni kumuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu jambo ambalo hana uwezo nalo isipokuwa Mwenyezi Mungu. Na katika shirki kubwa ambayo tunayaona leo ni kufanya tawaf kunyenyekea makaburi, kwenda kwa waganga na wachawi bali kuyaamini yote wanayoyasema kwa kudai mambo yaliofichika, na uhakika ni kwamba hakuna anayejuwa yaliofichika isipokuwa Mwenyezi Mungu na hakuna anayeweza kuleta madhara kumpata mtu isipokuwa Mwenyezi Mungu na hakuna anayeweza kuzuia kheri Akitaka Mwenyezi Mungu kuleta kheri hiyo.

قال تعالى) : وَإِنْ يَمْسَسْكَ اللَّهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ وَإِنْ يَمْسَسْكَ بِخَيْرٍ فَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ) [الأنعام: 17]

Amesema Mola (Subhaanahu wa Taala): {{Na Mwenyezi Mungu Akimpa mtu mtihani wa madhara (ugonjwa) hakuna Anayeweza kuuondoa isipokuwa yeye na akimpa neema (siha nzuri utajiri) hakuna awezaye kuiondosha kheri hiyo isipokuwa Mwenyezi Mungu}} [ Al-Anaam : 17]. Kwa hivyo, tujue ya kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye anayeleta manufaa na madhara, na kwa sababu hiyo yatakiwa Mwenyezi Mungu aogopewe haki ya kuogopewa.

- Na aina za shirki ni mtu kuomba dua kumuomba mtu jambo ambalo hakuna awezaye kulifanya isipokuwa Mwenyezi Mungu kama kuondoa ugonjwa. Huku tukijua ya kwamba dua ni ibada, kwa hivyo, ibada hiyo ya dua haifai kufanyiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu.

- Aina nyingine ya shirki kubwa ni ushirikina katika nia na makusudio, hii ni mtu kunuwia au kufanya ibada kwa kutaka au kukusudia mambo ya kidunia au wamuone kwamba yuwafanya ibada au watu wamsikie au apate sifa kwa watu.

قال تعالى (مَنْ كَانَ يُرِيدُ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيْهِمْ أَعْمَالَهُمْ فِيهَا وَهُمْ فِيهَا لَا يُبْخَسُونَ15 أُولَئِكَ الَّذِينَ لَيْسَ لَهُمْ فِي الْآَخِرَةِ إِلَّا النَّارُ وَحَبِطَ مَا صَنَعُوا فِيهَا وَبَاطِلٌ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ16) [هود15: 16]

Amesema Mola (Subhaanahu wa Taala): {{Anayetaka uhai wa dunia na mapambo yake tutawapa malipo ya amali zao hapa duniani na hawatapunguziwa kitu, hao ni wale ambaye hawatakuwa na chochote kesho akhera isipokuwa moto na yatabatilishwa yote waliyoyafanya na ni batili yote ambayo walikuwa wakiyafanya}} [Huud : 15 - 16]. Haya ni malipo ya wanaofanya ibada kwa ajili ya kuonekana na watu na kwa ajili ya dunia.

- Aina nyingine ni shirki ya kutii viongozi wa dini kinyume na miongozo sahihi ya Uislamu katika kuhalalisha vilivyoharamishwa na Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala).

قال تعالى : اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِنْ دُونِ اللَّهِ Amesema kuwatii

[التوبة: 31]wanaohalalisha vilivyoharamishwa: {{Wamewafanya wanavyuoni wao na wafanya ibada ni miungu kinyume}} [Tawba : 31]. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) Alimfasiria Adiy bin Hatiim ibada yenu kwao ni kumtii katika kumuasi Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala).

Shukrani za dhati zote zamstahiki Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe vyote. Rehma na amani zimfikie Kipenzi chetu Mtume Muhammad. Ama baada ya haya, napenda kuendelea kuzitaja aina za shirki nazo ni:

Aina za Shirki:

- Aina nyingine ya shirki ni kumpenda mtu au kitu zaidi kuliko Mwenyezi Mungu tena katika hali ya kumtukuza au kukitukuza kitu kile na kukidhalilikia.Na pindi mapenzi haya yafanyiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu basi ni shirki.

قال تعالى : (وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يَتَّخِذُ مِنْ دُونِ اللَّهِ أَنْدَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّهِ وَالَّذِينَ آَمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِلَّهِ ) [البقرة: 165]

Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala): {{Na katika watu wanawafanya wasiokuwa Mwenyezi Mungu kuwa wanavyompenda Mwenyezi Mungu na hakika walioamini wanampenda zaidi Mwenyezi Mungu}} [Al-Baqara : 165].

Kueni ndugu katika imani kwamba ukubwa wa dhambi la shirki kwani Mwenyezi Mungu hamsamehe anayemshiriksha endapo atafariki na dhambi hizo bila kumtaka yeye msamaha kwa kuwa Mola (Subhaanahu wa Taala) haridhii isipokuwa Tawhidi na pia haisamehe shirki. Kwa hivyo, adhabu ya mshirikina ni kubwa na atapata udhalilifu hapa duniani kabla ya kuadhibiwa kesho akhera.

قال تعالى) : إِنَّهُ مَنْ يُشْرِكْ بِاللَّهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنْصَارٍ) [المائدة: 72] Amesema Mola (Subhaanahu wa Taala): {{Hakika mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu amemuharamisha pepo na makazi yake ni motoni na hawatapata madhalimu wenye kuwasaidia}} [Al-Maaidah : 72].

Napenda tujiuze maswali yafuatayo;

Ni nani katika sisi hataki usalama duniani na kesho akhera?

Ni nani kati yetu hataki kuingia peponi bila ya hesabu?

Ni nani kati yetu hataki kupata uhai mzuri duniani na kuokoka siku ambayo haitofaa mtu mali yake wala watoto isipokuwa atayenda kwa Mwenyezi Mungu kwa moyo uliyosalimika na madhambi?

Jawabu la maswali tuliyoyauliza kuitekeleza Tawhidi katika maisha yake yote. Kubwa linalotakiwa ni mtu kujifundisha mambo yanayofungamana na Tawhidi vizuri kuyatilia umuhimu mkubwa katika maisha yake kwa kusoma vitabu vya Tawhidi na kusikiliza darasa za wanavyuoni walioshikamana na Tawhidi na sunna, kwani kufanya hivyo ni nuru katika nyoyo. Na vile vile kuvisoma vitabu vya Tawhidi ili kujua Tawhidi ni nini Tawhidi,sababu za shirki,hukmu za shirki na dalili za hukumu za shirki hizo, kuyajuwa hayo ni mwangaza ili mtu asibaki katika giza la shirki, na Tawhidi pia hutengeneza moyo wa mtu na jamii kwa jumla.

Enyi ndugu katika imani! Msihadaike na dunia na kuipuuza Tawhidi iliyokusanya kila kitu na kila mafanikio duniani na kesho akhera na kwa ajili ya Tawhidi wametumlizwa Mitume wote na kuumbwa pepo na moto. Nawausia ndugu zangu Waislamu mulipe suala hili la Tawhidi kipaumbele katika maisha yetu, na muikabili Tawhidi kwa nia njema na nia ya kweli. Na haifai kulipuuza kwa hali yoyote kwani atayelipuuza suala hili yuko katika hatari kubwa duniani na vile vile kesho akhera.

Mwisho

Twamshukuru Mungu tumegusia nukta muhimu kwa kubainisha umuhimu wa Tawhidi na kwamba Tawhidi ni sababu kubwa ya kuokoka mwanadamu siku ya kiama kupata msamaha pia tukabainisha kwamba Tawhidi ni sababu ya kuondoshewa balaa na fitna na mwisho tumebainisha umuhimu wa kujifundisha Tawhidi na shirki kwa aina zake.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Azitengeneze nia zetu katika vitendo vya kila siku na azitengeneze ibada zetu za kwa jumla, pia Aitengeneze Dini yetu na dunia yetu kwani yeye ni muweza wa kila kitu.





Vitambulisho:




Kuzuru Madina: fadhila zake na utukufu wake