Miongoni mwa misingi ya kisheria ni kufunga mlango wa fitna. Na miongoni mwa Rehma za Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni kufunga mlango wa shari, basi mwenye kufungua mlango huo atapata madhambi. Amesema mshairi:- Ikiwa mja hatovaa vazi la ucha Mungu, atakuwa uchi hata kama amevaa nguo. Na mja mwema ni yule amchaye Mola wake, wala hakuna ubora kwa anaye muasi Mola wake.
Ndugu Waislamu, Leo tunashuhudia wazi kabisa namna wanawake wanavyo dhihirisha mapambo yao, na kutovaa hijabu. Na bila shaka, kitendo hiki ni katika madhambi makubwa, na ni sababu ya kuteremshwa adhabu duniani, na kupata adhabu kali siku ya kiama. Ndugu zangu Waislamu, kuweni na adabu ya Mwenyezi Mungu na muwalazimishe wake zenu kuvaa hijabu na kusitiri miili yao kama alivyo amrisha Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) katika Qur’an tukufu.
Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال عز وجل ) يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُلْ لِأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِنْ جَلَابِيبِهِنَّ ذَلِكَ أَدْنَى أَنْ يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَحِيمًا ) [الأحزاب: 59]
{{Ewe Mtume, Waambie wake zako, na binti zako, na wanawake wa Kiislamu, wajiteremshie vizuri nguo zao. Kufanya hivyo kutapelekea upesi wajulikane kuwa ni watu wa heshima ili wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe na Mwingi wa kurehemu}}.
Jukumu la kila Muislamu kupiga vita Fitna ya Wanawake
Enyi Waislamu mcheni Mwenyezi Mungu na katazeni wanawake wenu na binti zenu kudhihirisha mapambo yao. Ni lazima kila Muislamu abebe jukumu la kuamrisha mema na kukataza mabaya. Kwani, tukiacha kufanya hivyo, tutalaaniwa na Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) kama walivyo laaniwa watu waliotangulia. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Watu wakiona uovu na wasiukataze uovu huo huhofiwa kuwateremkia adhabu ya Mwenyezi Mungu].
Amesema Mwenyezi Mungu (SW ):
قال عز وجل ) : لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَى لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ذَلِكَ بِمَا عَصَوْا وَكَانُوا يَعْتَدُونَ78 كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَنْ مُنْكَرٍ فَعَلُوهُ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ) [المائدة: 79]
{{Walilaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa Israil kwa ulimi wa Daudi na Isa bin Maryam. Hayo ni kwa sababu waliasi wakipindukia mipaka. Hawakuwa wenye kuzuiana (kukatazana) mambo mabaya waliyokuwa wakiyafanya. Uovu ulioje wa jambo hili waliokuwa wakifanya}}.
Na amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Atakaye uona uovu na auzuie kwa mkono wake, asipoweza kwa ulimi wake, asipoweza kwa moyo wake na ni udhaifu wa imani].
Ndugu katika imani, Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Amewaamrisha wanawake kuvaa hijabu na kubakia majumbani mwao, na kutolegeza sauti zao. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال تعالى) يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍ مِنَ النِّسَاءِ إِنِ اتَّقَيْتُنَّ فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَعْرُوفًا 32وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَى وَأَقِمْنَ الصَّلَاةَ وَآَتِينَ الزَّكَاةَ وَأَطِعْنَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّهُ لِيُذْهِبَ عَنْكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا) [الأحزاب: 33]
{{Enyi wake wa Mtume, nyinyi si kama yoyote tu katika wanawake wengine. Kama mnataka kumcha Mwenyezi Mungu, basi msiregeze sauti zenu ili asitamani mtu mwenye ugonjwa moyoni mwake, na semeni maneno mazuri. Na kaeni majumbani mwenu, wala msionyeshe mapambo yenu kama walivyo kuwa wakionyesha mapambo yao wanawake wa zama za ujahili}}.
Masharti ya Hijabu:
Kufunika mwili wote isipokuwa uso
Hijabu isiwe na mapambo juu yake
Hijabu iwe nzito wala isiwe yenye kuonyesha mwili
Hijabu iwe pana wala isiwe yenye kubana mwili
Hijabu isiwe na manukato
Hijabu isifanane na vazi la mwanamume
Hijabu isifanane na vazi la makafiri
Hijabu isiwe ni vazi lenye kujulikana
Ushahidi wa masharti yaliyopita, Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال تعالى (يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُلْ لِأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِنْ جَلَابِيبِهِنَّ ذَلِكَ أَدْنَى أَنْ يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَحِيمًا ) [الأحزاب: 59]
{{Ewe Mtume, Waambie wake zako, na binti zako, na wanawake wa Kiislamu, wajiteremshie uzuri nguo zao. Kufanya hivyo kutapelekea upesi wajulikane kuwa ni watu wa heshima ili wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe na Mwingi wa kurehemu}}.
Na Akasema tena Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال تعالى (وَقُلْ لِلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَى جُيُوبِهِنَّ) [النور: 31] {{Na waambie Waislamu wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa yanayodhihirika. Na waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao}}.
Amesema Mtume (Subhaanahu wa Taala): [Watu wawili ni watu wa motoni, mmoja wao ni mwanamke aliyevaa nguo lakini yuko uchi].
Na akasema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) [Mwanamke yoyote atakaye jitia manukato na akapita mbele ya watu, ili watu wasikie harufu ya mafuta yake, basi mwanamke huyo ni mzinifu].
Amesema tena Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Amemlaani Mtume wa Mwenyezi Mungu mwanamke mwenye kuvaa vazi la mwanamume, na mwanamume mwenye kuvaa vazi la mwanamke].
Na amesema tena Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Atakaye jifananisha na watu basi ni katika wao].
Na amesema tena Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Atakae vaa vazi la kujionyesha, Mwenyezi Mungu Atamvisha vazi la udhalili siku ya kiyama].
Ndugu katika imani, ni wajibu juu kila mwanamume kuhakikisha masharti ya hijabu wakati anapo mnunulia mke wake au binti yake vazi la kuvaa. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Nyinyi wote ni wachunga, na kila mmoja ataulizwa juu ya kile alichokichunga]. Inatupasa kumuogopa Mola wetu na kutekeleza majukumu yetu kama alivyo tuamrisha Mwenyezi Mungu.
Sababu ya Uharibifu wa Wanawake
Ndugu Waislamu, inajulikana wazi ya kuwa wanawake wa leo wamezidi kuonyesha umbile lao na mapambo yao. Kuna sababu nyingi ambazo zimechangia kupatikana uharibifu katika jamii. miongoni mwasababau hizo ni:-
Mwanamke kukaa faragha na mwanamume ambaye si maharimu yake. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Hawatokaa faragha mwanamke na mwanamume isipokuwa shetani huwa watatu wao].
Kusafiri peke yake. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Asisafiri mwanamke isipokuwa awe na mahrimu yake (Wasioruhusiwa kumuoa) Wala asikae faragha mwanamke na mwanamume].
Wanawake wa kiislamu kujifananisha na wanawake wa kikafiri. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Atakaye jifananisha na watu basi ni katika wao].
Wajibu wa Viongozi na Mahakimu na Wanavyuoni
Enyi waja wa Mwenyezi Mungu, mcheni Mola wenu na tahadharini kwa mambo aliyoyaharamisha, na saidianeni kwa mambo mema na msiache kwa mambo ya haki na kusubiri. Na jueni ya kuwa Mwenyezi Mungu atawalipa kwa mambo mliyoyafanya. Na inalazimu kwa viongozi wa nyanja tofauti kutonyamaza katika kuondosha uovu.
Imepokewa kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Hakutumilizwa Nabii isipokuwa alikuwa na wafuasi na wenye kuchukua uongozi wake, kisha wakawayapa mgongo yote yaliyokuja baada yake, wanazungumza mambo wasiyoyafanya, na wanafanya mambo wasiyoamrishwa, atakae pigana nao kwa mkono wake, basi huyo ni muumini. Atakaye pigana nao kwa moyo wake basi huyo pia ni muumini, wala hakuna baada ya ya hapo chembe yoyote ya imani (mkono, ulimi na moyo)].
Wito kwa Wanawake Wakiislamu
Muogope Mwenyezi Mungu! Ewe mtoto wa kike
Muogope Mwenyezi Mungu! Mwenye kujipamba na kwenda sokoni
Muogope Mwenyezi Mungu! Mwenye kuvaa hijabu kama pambo wala si kwa kujistiri
Muogope Mwenyezi Mungu! Kwa kile alichokukalifisha, ambapo mbingu na ardhi imekataa kubeba.
Muogope Mwenyezi Mungu! Na hifadhi nafsi yako.
Muogope Mwenyezi Mungu! Na kutangamana na wanaume na kutoka bila ya maharim
Muogope Mwenyezi Mungu! Ewe Mwenye kuingia kwa matibabu bila maharim.
Muogope Mwenyezi Mungu! Ewe mwenye kuwalea watoto wako malezi ya wanyama.
Muogope Mwenyezi Mungu! Ewe mwenye kujitia manukato.
Muogope Mwenyezi Mungu! Na mrejee katika uongofu, jua kama adhabu kali mbele ya Mwenyezi Mungu, na dunia si makazi.
Mwisho
Ndugu Waislamu, Na kariri tena kwa kuwakumbusha jukumu kubwa tulilo beba nalo ni kuwasimamia wanawake na kuwaamrisha mema na kuwakataza mabaya. Fitna kubwa leo ulimwenguni ni fitna ya wanawake, na maadui wanawatumia wanawake kama njia ya kufikia malengo yao. Jamii nyingi zimeharibikiwa kwasababu ya kuharibika mwanamke. Kwa hivyo, Ni lazima kila Muislamu ajitolee kwa hali na mali kuwahifadhi wanawake katika jamii yetu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awahifadhi mabanati wa kiislamu kutokana na vitimbi vya wenye kufanya vitimbi.
Ewe Mwenyezi Mungu wakusanye wao katika imani na kuwapa pepo siku ya akhera Mwenyezi Mungu sitiri aibu zetu na utuhifadhi mbele yetu, nyuma yetu na upande wa kulia na upande wa kushoto na juu yetu.