KUAMINI MAKADIRIO YA MWENYEZI MUNGU


3159
wasifu
Hakuna raha wala utulivu kwa mja katika dunia hii isipokuwa ni kule kuamini kwake mapitisho ya Mwenyezi Mngu na makadirio Yake. Nako ni kuamini kuwa chochote Anachotaka Mwenyezimngu kiwe ni chenye kuwa na asichoikitaka hakiwi, na kwamba lau watu wote watajikusanya kumdhuru mtu kwa chochote hawaweza kumdhuru isipokuwa kwa kitu Alichomwandikia Mwenyezi Mngu, na lau watajikusanya kumnufaisha kwa chochote, hawataweza kumnufaisha isipokuwa kwa kitu alichomwandikia Mwenyezi Mngu.

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu aliyeumba kila kitu kwa kadari yake na na shahudia ya kwamba hapana Mola Apasae kuabudiwa kwa haki ila Yeye, hana mshirika katika uumbaji wake. Na nashuhudia ya kwamba Mtume Muhammad ni mja wake na ni Mtume wake. Swala na Salamu zimshukie Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) Ambaye alifikisha ujumbe na akatekeleza amana na akapigana katika njia ya Allah haki ya kupigana mpaka yakamfikia yeye mauti.

Ni lazima kwa kila Muislamu kuwa na itikadi ya kwamba kheri na shari ni kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na ujuzi wake na mapendeleo yake, lakini kufanya kheri na shari kwa mja ni kwa khiyari yake na uchungaji wa jambo na makatazo ni wajibu kwa mja haifai kumuasi yeye Mwenyezi Mungu kisha kusema Mungu amenikadiria.

Mazungumzo yetu leo ni makubwa yanatokana na nguzo moja katika nguzo za imani sita, ambayo mwenye kukanusha nguzo hiyo Mwenyezi Mungu hamkubalii yeye na haitimu imani ya mtu ila kwa kuamini kadari. Nguzo hii ni kubwa, mwenye kuwa nayo hupata utulivu na kujibu masuali mengi na mwenye kulemewa nayo huwa hapati kitu.

Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

(إنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ )[القمر: 49]

{{Hakika kila kitu tumekiumba kwa kadari}} [Al-Qamar:49]. Na Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

وقال سبحانه) : (سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى1 الَّذِي خَلَقَ فَسَوَّى 2وَالَّذِي قَدَّرَ فَهَدَى3)

[الأعلى1: 3]{{Litukuze jina la Mola wako aliye mtukufu, aliyeumba akatengeneza na akakadiriya (kila jambo)} [Al-A’alaa : 1 - 3]. Na imethibiti katika sahihi ya kwamba Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) alikuwa na masahaba zake, akamjia Jibril kwa sura ambazo si zake kwa sura za mtu katika watu akamuuliza kutokana na masuali ya Dini. Katika masuali hayo; “Akamuambia imani ni kuamini Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume yake na Siku ya Mwisho na kuamini Kadari kheri yake na shari yake. Akasema Jibril: umesema kweli. Mwisho wa hadithi Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) Akawaambia waliokua naye: Je mnajua aliyekua akiuliza? Wakasema Mungu na Mtume wanajua zaidi, Akawaambia huyu ni Jibril amekuja kuwafundisha Dini yenu” (imepokewa na Muslim). Hadithi hii ina Tufundisha kujua nguzo sita za imani na yaliyokusanyika katika nguzo hizo nayo ni dini

Enyi Waislamu, Kadari ni ilimu ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) iliyotangulia vitu kabla ya kuandikwa, aliyo pambanuliwa kuwa yatakuwa. Hivyo basi ni kabla ya kuumbwa mbingu na ardhi kwa miaka khamsini elfu. Na uhakika wa kuamini kadari una dhamini mambo manne:

Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) ameumba kila kitu kwa kadari.

Kila kitu kimeandikwa kwenye (lawhul-mahfudh)

Ujuzi wa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) kujua kila kitu.

Kila kitu ni katika mapenzi ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala).

Kwa hivyo, kuamini kadari ni kuamini ujuzi wa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) wa kila kitu kabla ya kufanyika. Na halifanyiki jambo lolote nje ya ufalme wake. Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) anayo ilimu ya kila kitu. Ni wajibu kwa kila Muislamu kuamini ya kuwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) ameandika makadario ya viumbe vyote katika ubao uliohifadhiwa kabla ya kuumba mbingu na ardhi kwa miaka Khamsini elfu kama ilivyothibiti katika Hadithi iliyo sahihi, na kama alivyotoa khabari Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) katika kitabu chake:

وقوله :(إِنَّ ذَلِكَ فِي كِتَابٍ إِنَّ ذَلِكَ عَلَى اللَّهِ يَسِيرٌ) [الحج: 70]

{Hakika hilo liko kaitka kitabu na hakika hilo ni jepesi kwa Mwenyezi Mungu}. Kuamini kadari ni kuamini jambo lolote Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) akitaka linakua na mabalo halitaki liwe halitakua. Analolitaka liwe halina budi liwe na matakwa yote yako chini ya matakwa ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Na hamutaki jambo likawa ila atake Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala), wala hamuwezi katika jambo asipotaka Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala), Yeye ni mjuzi Mwenye hekima.

Jua Ewe Muislamu ya kwamba, itikadi ya Jabriya haina mahala katika Uislamu. Na katika akida ya Muislamu; Mwanadamu ni mwenye kuchaguzwa na hakua ni mwenye kwenda na maamrisho na makatazo bali anachagua ima achague njia ya kheri au njia ya shari.

Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala).

وقوله) : وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ) [البلد: 10]

{{Na tukambainishia zote njia mbili, ilio njema na ilio mbaya}} [Al-balad:10]. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) :

وقوله : (قَدْ أَفْلَحَ مَنْ زَكَّاهَا 9وَقَدْ خَابَ مَنْ دَسَّاهَا10) {{Hakika amefaulu mwenye kujitakasa nafsi yake na amepita patupu mwenye kuchafua nafsi yake}} [ Ashamsu 9-10]. Na ilmu ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) iliyotangulia na maandishi yake hayakuwa ni yenye kuungwaungwa na katika hilo ni kwasababu ya kusimamisha hoja juu ya waja na halipatikani jambo lolote ila Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) analijua kwa ukamilifu wa ilmu yake.

Na kama tunavyo jua baadhi ya watu wanafanya maasi kisha wanategemezea kadari. Haifai kutegemezea kadari pindi unapo fanya makosa. Si sawa mwanadamu kuchukua hoja kwa kadari juu ya kufanya maasia. Na kuna mengi sana kuhusu kuamini kadari lakini kwa sababu ya wakati tutakoma hapa. Mwenyezi Mungu atuafikie kila la kheri na atuepushe na kaila shari.

Shukurani zote ni za Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Aliye mfalme wa mbingu na ardhi. Utakatifu ni wake Bwana wa walimwengu wote na rehma na amani zimshukie Mtume Muhammad alietumilizwa na rehma kwa viumbe. Na baada ya yote. Tutakugusia matunda ya mwenye kuamini kadari na kufuata sababu za kisheria katika kutekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala).

Matunda ya kuamini kadari

Enyi waislam hakika matunda ya kuamini kadari kama ifuatvyo:-

Ni kumtegemea Mwenyezi Mungu Aliye Mtukufu. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) : مَا أَصَابَ مِنْ مُصِيبَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّهِ وَمَنْ يُؤْمِنْ بِاللَّهِ يَهْدِ قَلْبَهُ وَاللَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ) [التغابن: 11]

.

{{Haukufiki msiba ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na anaye muamini Mwenyezi Mungu huongoza moyo wake.Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu}} [Taghabun : 11]. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

وقال) : مَا أَصَابَ مِنْ مُصِيبَةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي أَنْفُسِكُمْ إِلَّا فِي كِتَابٍ مِنْ قَبْلِ أَنْ نَبْرَأَهَا إِنَّ ذَلِكَ عَلَى اللَّهِ يَسِيرٌ )[الحديد: 22]

{{Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwisha andikwa katika kitabu kabla hatujaumba. Na hilo kwa Asema Mwenyezi Mungu ni lepesi}} [Al-Hadid : 22].

Ni kujua mja kila linalompata haliwi ni lenye kumkosa, madamu limekwisha andikwa lazima limfikie. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Jua lau watu wote watakusanyika ila wakuletee madhara hawatakudhuru ila kwa jambo alilo kuandikia Mwenyezi Mungu, na lau watu wote watakusanyika ili wakunufaishe hawatakunufaisha kwa jambo lolote ila kwa jambo alilokuandikia Mwenyezi Mungu].

Kupatikana utulivu wa moyo, kama ilivyokuja katika Aya. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

وقال تعالى) : الَّذِينَ آَمَنُوا وَتَطْمَئِنُّ قُلُوبُهُمْ بِذِكْرِ اللَّهِ أَلَا بِذِكْرِ اللَّهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ )[الرعد: 28].

{{Wale waliyo amini na zikatuliya nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Sikilizeni, kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu nyoyo hutulia}}.

Mwisho

Muogopeni Mwenyezi Mungu waja wa Mwenyezi Mungu. Na muamini kadari ya Mwenyezi Mungu, na mufuate mwito wa Allah (Subhaanahu wa Taala). Hio ni njia ya peke yake itakayo wafikisha kwa Allah (Subhaanahu wa Taala). Ndugu Waislamu tuombeni uongofu kotoka kwake, na tujue haifai kutoa hoja kwa kadari, mfano kufanya maasiya kisha ukategemeza kwa Mwenyezi Mungu, au kusema Mungu hakunijaaliya kufanya jambo Fulani. Haya ni katika madhambi makubwa kwa kumnasibishia Mwenyezi Mungu jambo uovu.

Ewe Mwenyezi Mungu tunakuomba katika kisimamo chetu hiki na katika kuongojea faradhi miongoni mwa faradhi zako ulizo faradhia juu yetu, utupendeze sisi imani na utengeneze katika nyoyo zetu, utuepusha nakila lenye kuharibu imani zetu. Ewe Bwana wa walimwengu wote tusamehe zambi zetu na utujaalie ni katika wenye kusikia mema pamoja na kuyafuata.





Vitambulisho:




Kutayamamu