MAISHA YA UHAKIKA NI MAISHA YA AKHERA


4432
wasifu
maisha ya uhakika ni maisha ya akhera,ambapo hakuna kufiwa wala ugonjwa,wala dhiki za kimaisha,lakini hapa duniani ni starehe chache,na ni mda mchache kisha utakuwa ni mwenye kuondoka,kwa yule mwenye akili ni kujitahidi kutenda yatakao mfaa bada ya kufa kwake ili apate maisha ya uhakika na starehe ya daima

Himidi zote ni za Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. Na nashuhudia kwa moyo na kutamka kwa ulimi ya kwamba hapana apase kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah (Subhaanahu wa Taala) hana mshirika. Na nashuhudia kwa moyo na kutamka kwa ulimi ya kuwa Mtume Muhammad ni mja wake na ni Mtume wake. Na Sala na Salamu zimfikie Mtume Muhammad pamoja na Jamaa zake na Sahaba zake. Baada hayo, na wausia pamoja na kujiusia nafsi yangu kumuogopa Mwenyezi Mungu. Kwani kumuogopa Mwenyezi Mungu ndiyo sababu peke ya kutufanya sisi tuingie katika pepo ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala).

Ni ipi siku ya mwisho? Siku ya mwisho ni siku ambayo mwanadamu huacha dunia na kila kilicho chake na vitu vyote avipendavyo, na kuhamia nyumba ya mchanga, nyumba yenye giza nyumba ya wadudu iliyo na dhiki. Kukunjuliwa nyumba hiyo inategemea vitendo vyako. Kama ilivyo kuja kaburi ima inakua na bustani katika mabustani ya pepo au ni shimo katika mashimo ya motoni.

Enyi waja wa Mwenyezi Mungu, kila kilicho na uhai mwisho wake ni kufa. Na huu ni mwisho wa kila kiumbe sawa binadamu au mnyama, hakuna khiyari wala hakuna kuchagua upende usipende. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ 26وَيَبْقَى وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ 27)[الرحمن26: 27]

ardhi na mbingu kitatoweka. Na itabaki dhati ya Mola wako Mwenye utukufu na hishima}} [ Arrahmaan : 26-27]. Kwa hivyo, Mwanadamu ana nyumba mbili; nyumba ya mapito na kuondoka, na nyumba ya kubaki milele nayo ni nyumba ya akhera. Na nyumba ya akhera ndiyo nyumba ya utulivu na kubaki milele. Na ulimwengu namna utakao kua mrefu mwisho wake ni kumalizika. Kwa hivyo, mwenye akili ni yule ambae ameuangalia ulimwengu kisha akaupa mgongo, akaufanya ni mahali pa kupanda mbegu na akachukua zawadi za kumsaidia akhera. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) : اعْلَمُوا أَنَّمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا لَعِبٌ وَلَهْوٌ وَزِينَةٌ وَتَفَاخُرٌ بَيْنَكُمْ وَتَكَاثُرٌ فِي الْأَمْوَالِ وَالْأَوْلَادِ كَمَثَلِ غَيْثٍ أَعْجَبَ الْكُفَّارَ نَبَاتُهُ ثُمَّ يَهِيجُ فَتَرَاهُ مُصْفَرًّا ثُمَّ يَكُونُ حُطَامًا وَفِي الْآَخِرَةِ عَذَابٌ شَدِيدٌ وَمَغْفِرَةٌ مِنَ اللَّهِ وَرِضْوَانٌ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ) [الحديد: 20]

{{Jueni ya kwamba maisha ya kilimwengu ni mchezo na upuzi na mapambo na kujifakhirisha kwa mali na watoto. Ni kama mfano wa mvua iliyo mvutia mkulima mimea yake kisha ikabadilika rangi ya kawa rangi ya manjano kisha yakawa mabuwa. Na akhera kuna adhabu kali, na msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi zake. Na hayakuwa maisha ya kilimwengu ili na starehe ya kudanganya}} [ Al- Hadid :20]. Tunaona ya kwamba maisha ya ulimwengu ni maisha ambayo yana malizika hayaendelei ni kama mfano wa mmea unanawiri kwa masiku machache baadaye yanabadilika, baada ya kuwa na nguvu na rangi mzuri ya kuvutia. Na. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

وقال) : إِنَّمَا مَثَلُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنْزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ مِمَّا يَأْكُلُ النَّاسُ وَالْأَنْعَامُ حَتَّى إِذَا أَخَذَتِ الْأَرْضُ زُخْرُفَهَا وَازَّيَّنَتْ وَظَنَّ أَهْلُهَا أَنَّهُمْ قَادِرُونَ عَلَيْهَا أَتَاهَا أَمْرُنَا لَيْلًا أَوْ نَهَارًا فَجَعَلْنَاهَا حَصِيدًا كَأَنْ لَمْ تَغْنَ بِالْأَمْسِ كَذَلِكَ نُفَصِّلُ الْآَيَاتِ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ) [يونس: 24]

{{Hakika maisha ya ulimwengu ni kama mfano wa mvua inayo nyesha kutoka mawinguni ikaotesha mimea inayo toka aridhini vinavyo liwa na watu na wanyama ulipo kamilika uzuri wake, na ikapambika wakadhani wenye makulima hayo wanaweza juu yake, ikaja amri yetu mchana au usiku yakawa kama yaliyo vunwa kama kuwa hayakuwa jana. Hivi tunawafafanuliya alama zetu wakafahamu watu wanaofikiri}} [ Yunus : 24]. Mwenyezi Mungu Atupigia mfano wa ulimwengu na mvua inayo nyesha ikaotesha mimea ikawa ni chakula cha watu na wanyama. vile vile Mwenyezi Mungu Akapiga mfano wa mmea hunawiri kawa muda fulani bada ya muda inabadilika.

Na katika kuonyesha udhaifu wa ulimwengu ni maneno yanayo fuatia.

Imetokana na Ali Bin Abi Twalb akisema : unaondoka ulimwengu ukipa mgongo na inaondoka akhera ikikulekea. Na kila mmoja ana watoto, kuweni watoto wa akhera, msiwe watoto wa ulimwengu. Hakika leo ni vitendo hakuna malipo na kesho ni malipo hakuna vitendo.

Hapa anatuonesha Swahaba Ali Bin Abi Twalib mfano wa dunia ni kama ulimwengu unaondoka kwa kukupa mgongo. Kwa maana ya kunaondoka ulimwengu ni kuuwacha ulimwengu, na akhera inakufuata kwa kukupa uso. Halafu tukabainishiwa vile vile, mtu ambae hamu yake itakuwa ni ulimwengu basi Mwenyezi Mungu Atajaalia umasikini mbele ya macho yake.

Imetokana na Zeydi Bin Thaabit radhi za Mwenyezi Mungu juu yake Amesema: Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Ambae ulimwengu utakuwa hamu yake Mwenyezi Mungu Atayakata mambo yake na atajalia ufukara mbele ya macho yake, na hatampatia ulimwengu ila kile alicho andikiwa. Na yule ambae akhera ndiyo lengo lake Mwenyezi Mungu atalikusanya jambo lake na atajalia utajiri katika moyo wake na atampa ulimwengu] (Ibnu Majah). Hadithi hii, Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) anatupa mafundisho bora nayo ni kutokuwa na hamu ya ulimwengu, tushughulike na akhera zaidi. Kwani ulimwengu ni kitu cha kumalizika, lakini tushughulike na akhera zaidi ili tupate kufaulu ulimwenguni na akhera.

Enyi Waisilamu shindaneni kufanya vitendo vyema ili mupate kufaulu katika kuupata huo ulimwengu na akhera. Na watahadharisha na kuathirika na ulimwengu mtapata khasara ulimwenguni na akhera. Hakika ulimwengu ni mavuno ya akhera. Ambaye hakulima ulimwenguni hatovuna akhera.

Enyi Waislamu, hakika nyumba ya akhera ndiyo nyumba ya uhakika, ambayo mwanadamu atasema atakapo shuhudia uhakika wake: Natamani lau ningetanguliza maisha yangu ya dunia kuchuma maisha ya akhera. Kwasababu, maisha ya akhera ndiyo maisha bora mna kila kitu bora na watu hawatakufa wala hawatangonjeka, hakika hiyo ni nyumba ya amani nyumba isiyo na shida mna kila kinacho tamani nafsi.

Ubora wa Nyumba ya Akhera

Na katika ubora wa nyumba hiyo ni kama alivyo eleza Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam):

[Mahali pakuweka kibati peponi ni bora kuliko ulimwengu na vilivyoko ndani yake]. Ndiyo Amesema kweli Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Maisha ya akhera ni bora kuliko maisha ya ulimwengu, kulingamana na starehe zilizoko. Huko kuna wanawake wasio na aibu wameumbwa ni zawadi kwa wale watakao ingia peponi].

Na Akasema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) katika kusifu pepo:

قال تعالى ): فَأَمَّا إِنْ كَانَ مِنَ الْمُقَرَّبِينَ 88فَرَوْحٌ وَرَيْحَانٌ وَجَنَّةُ نَعِيمٍ89 )الواقعة: 88]

{{Ama wale walio kurubishwa na Mwenyezi Mungu ni raha na mabustani yaliyo jaa starehe}} [Al-Waqiah : 88 - 89]. Hivi ndivyo yatakavyo kuwa maisha ya akhera inayo takikana ni kusubiri. Na watu wa peponi watapewa watumishi wenye kuwatumikia hawataona jua wala baridi, watadhalilishwa matunda ya kila aina na vinywaji vya kila aina na vyombo watakavyo tumia ni dhahabu na fedha.

Enyi Waisilamu, shindaneni katika kufanya vitendo vya akhera ili mpate kwa hilo ulimwengu na akhera. Na watahadharisha na kuathirika na ulimwengu, mutakhasirika ulimwenguni na akhera. Hakika ulimwengu ni mapando ya akhera, ikiwa hukupanda katika ulimwengu kwa ajili ya akhera yako hakika umekhasirika akhera yako.

Enyi Waisilamu, hakika maisha ya nyumba ya akhera ndiyo maisha ya uhakika ambayo atasema mwanadamu atakapo shuhudia uhakika wake natamani ningetanguliza maisha yangu kwa ajili ya akhera. Hivyo basi ni kwamba maisha ya akhera ndiyo maisha watakaoishi watu hawatakufa. Watapata katika hiyo pepo kila wanacho kitaka macho yatafurahi hiyo ni nyumba ya amani iliyo salimika na kila upungufu na kila balaa hakuna magonjwa wala hakuna kufa wala hakuna kuzeeka.

Amesema Ibnu Rajabu katika kutafsiria hadithi ya Abdullahi Bin ‘Umar: «Kuwa katika ulimwengu ni kama mgeni:». Hadithi hii ni msingi wa kufupisha matarajio katika ulimwengu. Hakika Muisilamu hatakikani achukue ulimwengu ni mji na ni makao ya kutulia, lakini linalo takikana ni awe kama kwamba yuko safarini kwa maana ni mwenye kujiandaa na safari.

Mwenyezi Mungu atujalie ni wenye kuingiya peponi pamoja na Mitume na watu wema. Atupe mwisho mwema wakati wa kufa kwetu. Mwenyezi Mungu atujaalie ni wenye kushinda na katika kutafuta pepo. Atujaalie ni wenye kuingia katika pepo ya firdaus ya juu. Atujaalie ni katika wenye kuyasikia mema pamoja na kuyafuata. Atupe mema ya ulimwengu na akhera.

Himidi zote ni za Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mwenye kuneemesha mwalimwengu wote kwa jumla katika dunia na swala na salamu zimshukie Mtume Muhammad na Jamaa zake na Swahaba zake wote.

Enyi watu, yalipokua maisha ya akhera ndio maisha ya uhakika ya milele. Watu wema waliopita waliyafanya maisha ya kidunia ni mashamba kwa ajili ya akhera.

Amesema ‘Umar Bin Abdulaziz katika khutuba yake: ‘hakika ulimwengu sio nyumba ya utulivu ameandika Mwenyezi Mungu juu yake kumalizika kwa wakazi. Ni wangapi wenye kuamrisha kwa kuamini kupata mazao na muda mdogo yanaharibika na ni wakaaji wangapi wamefungamana na pahali hapo na baada ya muda mdogo wanapewa mahali hapo, fanyeni vizuri safari yenu kwa usafiri mzuri na chukua zawadi hakika zawadi bora ni uchaji Mungu.

Na alikua Habib Bin Muhammad kila siku akiusia wasia wa mwenye kufikiwa na mauti kumuosha yeye na mfano wake na alikua kila akiamka akilia au akichwewa na jua, mkewe akamuuliza kuhusu kilio chake akamwambia anaogopa akichwewa na jua asiamke na akiamka asichwe na jua. Alikua Muhammad Bin akitaka kulala akiwaambia watu wake awape salamu nyinyi, Mwenyezi Mungu, huenda kifo changu nisiamke. Hivi ndivyo ilivyokua kawaida yake. Na akasema Abubakar Muzni akiweza mmoja wenu asilale ila wasia wake uko chini ya kichwa chake basi na afanye hajui huenda akalala akiwa ni watu wa dunia au akawa ni katika watu wa akhira. Na alikua Aweso akiambiwa: vipi zama juu yako? Akisema vipi zama kwa mtu akifikiwa na jioni anadhani ya kuwa hataamka na akiamka hadhaani atafikiwa na jioni, ni mwenye kubashiriwa pepo au moto.

Enyi Waislamu hakika zawadi bora ni uchaji Mungu na mjue ya kwamba Mwenyezi Mungu amewaandalia waumini wenye kwenda mbio kujenga maisha mazuri katika ulimwengu na akhira. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) : مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِنْ ذَكَرٍ أَوْ أُنْثَى وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُمْ بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ )[النحل: 97]

7].

{{Mwenye kufanya mema sawa akiwa mume au mke naye ana imani tutampa maisha mazuri na tutawalipa thawabu zao kwa mema yao waliyoyafanya}} [Al-Nahal:97].

Mwisho

Mwisho, tujibidisheni kwa kutafuta maisha ya uhakika nayo sio mengine bali ya akhera. Tuishi maisha ya raha na tujiepushe na maisha ya ulimwengu tuweze kuvuna kesho akhera. Kama Alivyosema Mwenyezi Mungu: “Yoyote atakaye jiepusha nafsi yake na matamanio basi pepo ndio mashukio yake na marudio mema”. Mwenyezi Mungu Atujaalie ni wenye kukusanya zawadi njema zitufikishe kwake salama. Atupe mazuri ya ulimwenguni na ya akhera.





Vitambulisho:




Nguzo za Swala