MAPENZI YA MWENYEZI MUNGU (SW) NA MTUME WAKE (SAW)


3356
wasifu
Kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ni miongoni mambo ya Imani ya lazima. Mtu hawi Muislamu mwenye Imani mpaka atangulize mapenzi ya Mwenyezi Mngu na Mtume Wake mbele ya kila alichonacho, kiwe ni mali, mtoto, mzazi au watu wote, kama alivyoeleza Mpendwa Mteuliwa, rehema na amani zimshukie. Na kwa kadiri ya mapenzi ndiounapatikana utiifu na kufuata amri ya Mwenyezi Mngu na Mtume Wake, rehema na amani zimshukie.

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma alie mmoja hana mshirika wake hakuzaa wala hakuzaliwa. Na rehma na amani zimshukie kipenzi chetu na mwalimu wetu Mtume Muhammad na Jamaa zake na Sahaba zake wote.

Nini mapenzi? Mapenzi ni jambo ambalo watu wana shindana katika kupenda kitu. Mapenzi huonyesha ukweli wa mwenye kupenda kitu. Na tukisema kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume ni vIpi? Ni kufuata kila walilo amrisha na kuacha kila walilo kataza, kama ilivyo kuja katika Qur’an.

قال تعالى : (وَمَا آَتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانْتَهُوا) [الحشر: 7] Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala): {{Na anachokupeni Mtume basi pokeeni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho}} [ Al-Hashri:7]. Ndugu Waislamu, mazungumzo yetu leo ni makubwa inahitajika kwa kila mmoja wetu sisi, bali kuhakikisha yanayolazimu imani, hakuna imani kwa yeyote ambae hatahakikisha hilo, nalo si lingine ni Mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wetu (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) na kuwa weka mbele kuliko yoyote. Hakika mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake ni katika imani. Hawi muumini yoyote ila atangulize mapenzi ya kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuliko chochote alichokimiliki mali, watoto, wazazi na watu wote. Kama alivyo toa khabari juu ya hilo Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) : قُلْ إِنْ كَانَ آَبَاؤُكُمْ وَأَبْنَاؤُكُمْ وَإِخْوَانُكُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ وَعَشِيرَتُكُمْ وَأَمْوَالٌ اقْتَرَفْتُمُوهَا وَتِجَارَةٌ تَخْشَوْنَ كَسَادَهَا وَمَسَاكِنُ تَرْضَوْنَهَا أَحَبَّ إِلَيْكُمْ مِنَ اللَّهِ وَرَسُولِهِ وَجِهَادٍ فِي سَبِيلِهِ فَتَرَبَّصُوا حَتَّى يَأْتِيَ اللَّهُ بِأَمْرِهِ وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ) [التوبة: 24]

{{Waambie Muhammad ikiwa wazazi wenu na watoto wenu na ndugu zenu na wake zenu na mali zenu mliyoyachuma na biashara zenu mnazoogopea kuharibika na majumba yenu mnavyoyapenda (ikiwa vitu hivi) ni vipendi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kupigania dini yake, basi ngojeni amri ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu maasi}} [ Tawab : 24].

Amesema Kadhi ‘Iyadh: ‘ Inatosha Aya hii kuwa ni tanabahisho na ni dalili kubwa na ni huja juu ya ulazima wa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na kuonyesha uwajibu wake na ni haki kumpenda Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Wakati Mwenyezi Mungu Alipotangaza yoyote atakaye kuwa mali yake, watoto wake, mke wake ni bora kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume, kisha akawaahidi adhabu kali, kwa kusema: “ Ngojeni amri ya Mwenyezi Mungu ije. Kisha Akakamilisha Aya kwa kuwaita maasi, na Mwenyezi Mungu na hawaongozi mafasiki.

`وقال تعالى :(قُلْ إِنْ كُنْتُمْ تُحِبُّونَ اللَّهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ) [آل عمران: 31]

Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala): {{Waambie Ewe Muhammad, Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni mimi Mtume, hapo Mwenyezi Mungu atakupendeni na atawasamehe dhambi zenu}} [Al-Imran : 31].

وقال : (يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا لَا تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيِ اللَّهِ وَرَسُولِهِ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ) [الحجرات: 1]

Amesema tena Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala): {{Enyi mlioamini, Msitangulize kusema lenu mbele ya neno la Mwenyezi Mungu na Mtume wake; na mcheni Mwenyezi Mungu; hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia na mwenye kujua}} [Al-Hujrat : 1].

Na kama ilivyo kuja katika Hadith. Imepokelewa na Anas Akisema: Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Hawi na imani mmoja wenu mpaka anipende zaidi mimi kuliko mzazi wake na mtoto wake na watu wote]. Amepokea Anas kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akisema: [ Mambo matatu ukiwa nayo unapata utamu wa imani; Ni kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake zaidi kuliko wengine. Na asimpende mtu ila kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na achukie kurudi katika ukafiri kama anavyo chukia kuingia motoni].

Na mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake yanao alama za kujulisha mapenzi yao. Wamezitaja na wakazibainisha Wanachuoni, zimetolewa katika Qur›an na sunnah na miongoni wa alama hizo:

Alama za kujulisha Mapenzi kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)

Ni kufuata Kitabu cha Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala).

Ni kutekeleza Sunnah zake zote, kwa kumfuata Mtume na kufanya sunnah zake na kufuata maneno yake na vitendo vyake. Na kufuata maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake na kujipamba kwa adabu za Mtume katika uzito na wapesi. Amesema Qaadhi Iyadh: ‘Mwenye kupenda jambo huathirika na huathirika kwa kuliafiki. Asipokuwa hivyo, huwa si mkweli katika mapenzi yake.

Kuathirika na aliyoweka Mwenyezi Mungu na kujiepusha na mapenzi ya nafsi na kufuata matamanio.

Shukurani zote ni za Mwenyezi Mungu na mwisho mwema ni kwa wale wanao mcha Mwenyezi Mungu. Na hakuna anaye kiuka mipaka ya Allah isipokuwa ni dhalimu. Na kubali kwa moyo ni kutamka kwa ulimi ya kuwa hapana Mola Apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, Asiye na mshirika wake. Na kubali kwa moyo ni kutamka kwa ulimi ya kuwa Mtume Muhammad ni mja wa Mwenyezi Mungu na ni Mtume wake. Ewe Mwenyezi Mungu msalie Mtume wetu Muhammad, kama ulivyo msalia Nabii Ibrahim wewe peke yako unastahiki kushukuriwa.

Mifano ya Mapenzi ya Mtume

Amri Bin Al-‘Asi radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie yeye, Amesema: ‘ Hakuwa yoyote anapendeza zaidi kwangu kuliko Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Wala hakuwa mtukufu katika macho yangu kuliko yeye. Na sikua na jaza jicho langu kwake yeye kwa sababu ya hishima yake. Na lau ningetakiwa ni msifu yeye nisingeweza, kwasababu jicho langu halitosheki naye’.

Aliulizwa Ali bin Abi Twalib radhi za Mwenyezi Mungu zimshukiye yeye Mlikuwa mkimpenda vipi Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)? Akasema : [ Na aapa kwa Mwenyezi Mungu, ilikua tuna mpenda zaidi kuliko mali yetu na watoto wetu na wazee wetu na mama zetu na kuliko maji baridi kwa mwenye kiu].

Imepokewa kwa Bilal na Hudhayfa Bin Yamani na Ammar Bin Yasir walikuwa wakisema yalipo wa hudhuriya wao kifo : ‘kesho tutakutana na Muhammad na kundi lake’. Na kama tunavyo jua kuna mambo ya kipatikana hukuepusha na mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wako nayo:

Mambo yanayo Haribu Mapenzi Ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake

Nikuzusha katika Dini yake

Nikuacha maamrisho ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Mwisho

Ndugu katika Imani, kukamilisha mapenzi ya Mtume ni kushikamana na mafundisho yake pamoja na mafundisho ya Masahaba zake. Kama alivyosema katika wasia wake juu ya kushikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na mafundisho yake sahihi.

Ewe Mwenyezi Mungu tujaalie ni wenye kumpenda Mtume, mapenzi ya uhakika wenye tushikamane na mafundisho yake, utujaaliye ni wenye kuingia peponi pamoja na Mtume bega kwa bega.





Vitambulisho:




Yasser Salama