SIRI ZA IBADA YA HIJJA


6258
wasifu
Je, kuna yoyote aliye ishuhudia Hija na ukubwa wake, Imani na vile inavyotoa mwangaza, makundi mengi namna yanavyomtukuza Mwenyezi Mungu na kumhimidi? Mandhari ya Hija ni ya ajabu na ya kutisha, inawafanya Waumini wafurahi na wenye kumpwekesha wawe na nguvu, na wenye kughafilika wanashangaa.Hija ina maana gani kwenu nyinyi, enyi Waislamu!

Ibada ya hija haikuanza leo, ilianza toka zama za Nabii Ibrahim. Ni moja katika nguzo za Uislamu. Ni lazima kwa Muislamu kuhiji, akiwa anaweza na ikiwa atahiji ataona na atapata faida mbalimbali

Maana ya Hija na Siri Zake

Enyi watu, Je mumeona ibada ya Hijja na ukubwa wake? Je mumeona imani na nuru zake? Je mmeona mrundiko wa msamaha wake? Ni vipi msimtukuze Mwenyezi Mungu na kumsifu?. Maangalizi yake mazuri yakuvutia, wanafurahika waumini, wanatukuka wanaompwekesha, wanasemehewa wenye madhambi, wanasafika walioghafilika.

Maana ya Hija

Je inamaanisha nini hija. Enyi Waislamu? Sidhanii kwamba ibada hii kwako haina mawaidha, idadi kubwa ya watu inaenda hija na wengi wao wanasamehewa madhambi na wanabadilika kiimani, baadaye yeye eti asiathirike.

Enyi mabwana watukufu, hakika katika hija pana viwanja, pana kukusanyikana, pana minara yenye vyeo baada ya kudharauliwa, na lengo lake ni uende ukafute dhambi kabla hujafa. Inavyotakikana ni kwamba umma usisahau siri za hija. Miongoni mwa faida zake; ni kupata ufungamano wa kisawasawa na kujuana na kujadidisha imani na kuingia hamu na ghera ya kiibada na kuzidi kumcha Mungu.

Visimamo katika Aya za Hija

Enyi waja wa Mwenyezi Mungu, hakika Aya za sura ya hajj zinabeba siri na hikma za hajj lau tutazisoma kwa makini tutapata hivyo visimamo kama mafumbo na misemo, kama Mungu anavyosema katika maana ya Aya:

قال تعالى) : وَإِذْ بَوَّأْنَا لِإِبْرَاهِيمَ مَكَانَ الْبَيْتِ أَنْ لَا تُشْرِكْ بِي شَيْئًا وَطَهِّرْ بَيْتِيَ لِلطَّائِفِينَ وَالْقَائِمِينَ وَالرُّكَّعِ السُّجُودِ) [الحج: 26]

{{Tulipomtilisha nanga Ibrahim katika Makkah ili afanye makazi, tulimuusia asimshirikishe Mwenyezi Mungu, na aisafishe nyumba ya Mwenyezi Mungu kwa wenye kutufu na wenye kusimama, kurukuu, kusujudu katika kuswali}}.

Hakika kumpwekesha ndio tegemeo la mwanadamu, kila balozi katika nchi hii na ndivyo inavyotakikana na Mwenyezi Mungu. Na kama tutaishi kama anavyotaka Allah, tungetawala ulimwengu na wapinzani wa Allah watakuwa wanyonge.

Hakika kumpwekesha Allah kihakika ungetupelekea sisi tupate ulimwengu na watu wapate amani na ulinzi kutoka kwetu, hapo waja wangalimuabudu Allah, vilivyo na ushirikina ungeondoka, lakini sisi wenyewe wenye Tawhidi, tunayo matatizo, tuna kasoro nyingi, vipi tunaweza kuwa makhalifa wa Allah? Ama washirikina wataenda Jahannam.

Allah (Subhaanahu wa Taala) Amesema:

قال تعالى: (وَمَنْ يُشْرِكْ بِاللَّهِ فَكَأَنَّمَا خَرَّ مِنَ السَّمَاءِ فَتَخْطَفُهُ الطَّيْرُ أَوْ تَهْوِي بِهِ الرِّيحُ فِي مَكَانٍ سَحِيقٍ ) [الحج: 31]

{{Ambaye atamshirikisha Mwenyezi Mungu, ni kama kwamba anaporomoka kutoka mbinguni, na ndege wakanyakuwa au achukuliwe na upepo akaanguke pahali pa mbali}}.

Sisi Waislamu tunayo nafasi nzuri ya kuingia peponi na kuipata dunia. Al-Kaaba ilijengwa ili watu wahiji na ndani yake kuna jiwe jeusi. Maswahaba walikuwa na Tawhidi ya juu, mmoja ni ‘Umar ambaye amesema: ‘Mimi najua wewe ni jiwe hudhuru wala hunufaishi, na lau sikumuona Mtume anakubusu, nisingekubusu. Hii ina maana Muislamu ni ajue kuwa kutufu na kubusu na kuanzia na kumalizia, asifahamu kuwa kuna madhara au manufaa akivitekeleza na kumdhuru akiziacha, bali afahamu kuwa uchamungu wake ndio unaokusudiwa, ndio Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akamtuma Abubakar mwaka wa tisa aende hija, atangaze siku ya idi ya kuchinja kwamba washirikina wasije kuhiji wala wasije kutufu tuputupu sababu ya kumtukuza na kuheshimu ibada ya Mwenyezi Mungu na sehemu zake.

Mahali pa Ibada sio pa Kuchezea

Katika Aya za sura ya hajj zinatueleza kwa undani kuwa hapo hija ni pahali pa ibada takatifu, kwa sababu ibada hii ni ya msimu, na tuiheshimuni ibada hii ili mkiondoka hapa ili tuwe tumesafika na ambaye hatosafika ni ajilaumu mwenyewe, kwani adhabu iliyo huko akhera ni kali sana na sio mchezo.

Hija ni Mwalimu anayetufundisha kusaidiana

Aya za sura ya haji zinatuhimiza kusaidiana na kujitolea sana. Mola (Subhaanahu wa Taala) Anasema kumuambia Ibrahim awatagazie watu waje Hija, waone manufaa yao na wataje jina la Mwenyezi Mungu kwenye siku maalumu, kwa kumshukuru kwa kuwaruzuku wanyama na kuchinja ili wale wao wanyama na kulisha wenzao wenye umaskini na utajiri.

Hija inatukuza Thamani ya Taqwa

Enyi waja wa Mwenyezi Mungu, Hija inatia moyo upate uchaji Mungu zaidi, na athari zake utazipata kwenye Aya na hadithi. Kwa mfano Mola (Subhaanahu wa Taala) Anasema katika maana ya Aya:

وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ) [الحشر: 7] )قال تعالي :

{{Muogopeni Allah na mjue Allah ana adhabu kali}}.

Vile vile Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala) :

وقال أيضًا (ذَلِكَ وَمَنْ يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّهِ فَإِنَّهَا مِنْ تَقْوَى الْقُلُوبِ ) [الحج: 32]

{{Mwenye kumtukuza Allah hakika huyo ameshapata taqwa ya moyo}}. Huko mwendako ni akhera, bebeni zawadi, na zawadi za huko zitawafaa wenyewe, zawadi za huko ni taqwa, zawadi nyingine hazifai.

Amesema tena Allah (Subhaanahu wa Taala):

وقال سبحانة : (لَنْ يَنَالَ اللَّهَ لُحُومُهَا وَلَا دِمَاؤُهَا وَلَكِنْ يَنَالُهُ التَّقْوَى مِنْكُمْ) [الحج: 37]

{{Hazimfikii Mwenyezi Mungu nyama zenu wala damu zenu, kinacho mfika yeye ni uchaji Mungu kutoka kwenu}}.

Tukizisoma hizi Aya za hajj zinatuliza moyo kumcha Mmwenyezi Mungu, kufanya na kuepukana na mabaya. Ukifika hijja wajisikia wewe na wenzako muko sawa iwapo mumetoka miji mbalimbali, rangi mbalimbali, lugha mbalimbali, majumba mbalimbali, lakini yote hayo si kitu mpo pamoja kwenye hema, mnaswali Msikiti mmoja lugha za ibada zote ni moja, mavazi ni mamoja na ibada zote, mko pamoja katika twawafu, kusai na kadhalika.

Baada ya hija wajiona mko sawa umejuana na watu wengi, wajihisi mwenye kufanya ibada ndiye mbora kwa Mola kama alivyosema Mwenyezi Mungu na ndio tunamuona Suhayb Ar-Rumiyy na Salmaan Al-Faarisiyy walikuwa na cheo kikubwa mbele ya Mola wao kwa sababu ya taqwa mbele hata ya waarabu, hata Ammi ya Mtume Abu Lahab, kuondosha huo ubwana, Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). alipomuoa Zeinab binti Jahshi kwa Zeid ibn Harith, Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akaamrisha maswahaba wamuoze Abu Hind na waoe watoto wake.

Hija ni Muungano wa Kiislamu

Hija inatulingania tuwe Dini moja, malengo mamoja. Hii inaonekana wazi kwa wenye akili na wenye macho. Mahujaji wanakusanyana kwenye swala moja, uwanja mmoja na wanafunga mwezi mmoja. Kwa hivyo baada ya hajj tutakuwa na shabaha moja, hatutafaulu ikiwa hatutashikana sisi kwa sisi. Mola anatuonya ikiwa tutakuwa mbali mbali. Maadui wa Uislamu wanafurahika wakituona tuko madhehebu mbalimbali, ulinganizi wetu watafautiana, utawala wetu umegawanyika.

Allah (Subhaanahu wa Taala) Anasema:

قال تعالى : (وَلَا تَنَازَعُوا فَتَفْشَلُوا وَتَذْهَبَ رِيحُكُمْ) [الأنفال: 46]

{{Wala Msizozane msije mkaharibikiwa na kupoteza nguvu zenu}}.

Hija ni sehemu ya kujadidisha Imani

Katika maana ya hija ni kujadidisha imani na kutengeneza nafsi, kwa sababu imani za watu zinapanda na kushuka na watu hukumbana na fitna na vivutio. Kwa hivyo hutibiwa kwa Tawhidi na ibada na makosa aliyoyafanya yakafutika. Kama Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) alivyosema katika maana ya hadithi: [Mwenye kuhiji wala asifanye madhambi yoyote wakati wa kuhiji kwake, basi atarejea huko kwao akiwa hana dhambi hata moja kama siku aliyozaliwa na mamake]. Amepokea hadithi hii Bukhari na Muslim.

Maana ya hija ni kukumbusha akhera na siku ya kufufuliwa, kama Mungu anavyosema katika maana ya Aya:

قال تعالي : (رَبَّنَا إِنَّكَ جَامِعُ النَّاسِ لِيَوْمٍ لَا رَيْبَ فِيهِ) [آل عمران: 9]

{{Ewe Mola wewe ndiye wewe mwenye kuwakusanya watu siku hiyo isiokuwa na shaka}}. Siku ya ‘Arafa ni mfano mdogo ya siku ya kufufuliwa, watu hukusanyika kumtwii Mola na kufutiwa dhambi zao. Mkusanyiko wetu huo wa kiibada, hakujapatikana kuendesha ibada ya mkusanyiko vizuri namna hii. Ingawa tuna matatizo yetu ya ndani, lakini maadui wanatamani hivi.

Aliyepata bahati mbaya huenda haji kwa kujifakhiri na kujidai na iwapo huona fujo la watu, ibada tofauti tofauti, haathiriki kwa sababu ya riyaa. Huzidisha alikotoka na madhambi yake na hurejea yale yale madhambi yake, moyo wake umepotea, hakujaaliwa kuongoka na mwenye kudharauliwa na Mola hakuna mwenye kumtukuza.

Ulinganizi wa Habari Njema

Enyi ndugu zangu, wabashirieni umma wenu kheri, huu ni umma wa uadilifu na uongozi, inaongoza usalama na raha na kheri yote. Huu umma utakuja kuhukumu ulimwengu kwa kutumia Qur’an tukufu, Waislamu hawapo katika uongozi, bali wamepotea uongozi, ni giza na ujinga ulioenea na watu wamekosa mwangaza na ushindi. Kwa nini ikawa hivyo? Kwa sababu uongozi haupelekwi na wanaostahiki, wao ni waovu wanaongoza kwa hawaa na mapenzi ya nafsi zao; na hiyo ndio dini yao, akili zikaharibika, mawazo yakapotea, wakawaua wanadamu pasi na hatia. Huyo ndiye mwanadamu wa kimagharibi, au ndye aliyeendelea ambapo amefilisika roho na mawazo. Utafaulu vipi bila Dini? Utauongoza vipi ulimwengu pasina kuutengeza? Wao wako mbio kuua wanadamu, kutengeneza mabomu na vifaru, ati wao ndio wanatengeneza ulimwengu, wao ndio wanaotisha usalama wa ulimwengu na bidii yao kubwa ni ulimwengu uwaogope na wamesahau Allah amesema.

Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Amesema katika maana ya Aya:

قال تعالى) : يَعْلَمُونَ ظَاهِرًا مِنَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ عَنِ الْآَخِرَةِ هُمْ غَافِلُونَ) [الروم: 7]

{{Wanayajua maisha wanayoyaona, lakini kuhusu akhera wamesahau}}.

Utulivu unapatikana katika Dini

Hakika utulivu unaopatikana ulimwenguni ni hali palipo na Dini, na pakikosekana dini hakuna utulivu na msimu wa hija unatuelekeza kwenye Dini na nafsi zetu ziwe safi na zijiandae kubadilika, ili Mola naye atubadilishie hali zetu. Dini yetu katika ibada ya hija inahimiza kwa njia tofauti tofauti, Uchaji Mungu, umoja na kuhurumiana.

Jamii ambayo haina Dini huhesabiwa haina imani na iko mbali na Mola na ndipo Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akasema: [Watatu watapata ladha ya imani:- wa kwanza ni yule anayempenda Mungu na Mtume wake kushinda kitu chochote, wa pili ni yule anayempenda mwenzake kwa ajili ya Mungu tu, wa tatu, ni yule anayechukia kurejea kwenye ukafiri baada ya Mungu kumuokoa nao kama alivyo chukia kutiwa motoni].

Na Muislamu, imani imempatia yeye muongozo kwenye usawa na utulivu, inatakikana tushike mafunzo hayo kwa magego ili sisi wenye Dini tupambane na wasiokuwa na dini mpaka tuwarejeshe kwenye Dini na tuwache huru ili tupate kuingia kwenye kundi zuri la Mwenyezi Mungu ambalo ndilo kundi zuri. Na wale mahasidi wanaochukia ukweli aliowapa Allah na wakawa hawataki kusikia. Na lau wangesikia na wakawapelekea wenzao wangepinga vile vile. Na wale waja wema wameamini hawakalifishwi isipokuwa wawezalo, kwani ni waja wema na huwa wanashukuru kwa neema ya Uislamu walioupata na neema ya Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)

Mwisho

Enyi Waislamu wenzangu, tukumbukeni neema ya Uislamu, na kama si uislamu tungekuwa kwenye hasara. Mungu alituumba tufanye ibada, lakini makafiri wakafanya vile watakavyo mpaka akaja Mtume Muhammad (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akatufundiisha yale ambayo Mola anayataka na kuyapenda, kama mfano hija. Makafiri walikuwa wakiabudu watakavyo na ikawa hawalipwi na Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akatufundisha vile atakavyo Mola na kwahivyo, tunalipwa vizuri. Muislamu atasafiri kwa ndege au meli akiwa amejaa madhambi, lakini baada ya hija anarejea kwao akiwa amesafishika hana hata doa la dhambi, kwa hivyo biri utazipata kutoka kwa sheitwani.

Ewe Mwenyezi Mungu, tupe uwezo wa kwenda kuhiji, utuongezee imani na utukubalie hija zetu, ziwe ni hija zisizo na doa. Ewe Mola, tusamehe madhambi yetu.





Vitambulisho:




Binadamu wote ni sawa