Himidi zote ni za Mwenyezi Mungu tunamshukuru Yeye na tunaomba msaada kwake na tunaomba msamaha kwake. Tunajilinda kwake na shari za nafsi zetu na vitendo vyetu vibaya. Na Rehma na Amani zimshukie Mtume wetu Muhammad na Jamaa zake na Maswahaba wake wote.
Nini uchaji mungu?. Ni kujiepusha na kila ambalo Mwenyezi Mungu halitaki na kutekeleza kila jambo ambalo Mwenyezi Mungu analipenda. Vile vile, uchaji Mungu ni kujilinda na adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kufanya vitendo vizuri, na kuogopa kwa siri na kwa dhahiri. Na kuogopa. Ni kama alivyosema Ali Bin Abi Twalib: ‘ Ni kumuogopa Mola, na kutumia Qur’an, na kuridhika na kidogo, na kujianda kwa siku ya safari’. Imekuja ya kwamba ‘Umar Bin Khatwab radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie alimuuliza Ubayyah Bin Ka’ab: Taqwa ni nini? Akamwambia: Je umefuata njia ya miba? Akamwambia kwa nini? Hukujua? Akasema nilitembea kwa hadhari kuogopea miba kunidunga. Akasema hiyo ndiyo taqwa’.
Enyi Waislamu: na wausieni pamoja na kujiusia nafsi yangu kumuogopa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Kumuogopa Mwenyezi Mungu ni mkusanyiko wa kheri na mambo mengi yametajwa katika Qur’an tukufu. Hakuna kheri yoyote ya dunia na akhera wala ya ndani na nje ila Taqwa imeshikanishwa nazo. Na hakuna shari yoyote ya dunia na akhera wala ya ndani na nje ila Taqwa imekuwa mbali nayo. Na katika kheri za Taqwa ni kufunguliwa milango ya kheri, na kwa Taqwa hufunzwa usioyajua.
Jueni Enyi waja wa Mwenyezi Mungu; Taqwa ni wasia wa watu wa mwanzo na wa mwisho. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال تعالى :(وَلَقَدْ وَصَّيْنَا الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلِكُمْ وَإِيَّاكُمْ أَنِ اتَّقُوا( [النساء: 131] {{Na kwa hakika tuliwausia waliopewa kitabu kabla yenu, na nyinyi pia, kwamba mumche Mwenyezi Mungu}} [Nisaa : 131]. Na Taqwa ni Mwito wa Mitume na alama ya waja wema. Kila Mtume alikuwa akiwaambia watu wake:
قال تعالى) أَلَا تَتَّقُونَ )[الشعراء: 106]
{{Je hamumuogopi Mungu}} [Ashuraa :106]. Taqwa asli yake ni kinga baina ya mja na lile analoliogopa na kujitahadhari nalo. Na Mola wetu mtukufu ndiye Anaye stahiki kuogopewa nayeye pekee ndiye Anayetukuzwa. Kama Alivyosema Ali Radhi za Mwenyezi Mungu juu yake ‹Taqwa ni kumuogopa Mwenyezi Mungu na kutumia kitabuchake (Qur’an) na kutosheka na kichache na kujiandalia siku ya safari›.
Sifa za Wachaji Mungu.
Na inatulazimu sisi Enyi Waislamu tusimame na sifa za wanaomuogopa Mwenyezi Mungu. Katika sifa za wanaomuogopa Mungu (Subhaanahu wa Taala):
Kuamini mambo ya siri (ghaib)
Kusimamisha Swala kwa wakati wake.
Kutoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Kuamini Aliyoteremsha Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala).
Kuwa na yakini na Siku ya Akhera. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال تعالى) : الم 1ذَلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ فِيهِ هُدًى لِلْمُتَّقِينَ2 الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْغَيْبِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنْفِقُونَ3 وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِمَا أُنْزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنْزِلَ مِنْ قَبْلِكَ وَبِالْآَخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ4 أُولَئِكَ عَلَى هُدًى مِنْ رَبِّهِمْ وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُون5.) ]البقرة1: 5]
{{Hiki ni kitabu hakina shaka ndani yake ni ongofu kwa wanaomcha Mwenyezi Mungu. Ambao huyaamini yasioonekana na husimamisha swala na hutoa zile tulizowapa. Na ambao wanaamini yaliyo teremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako na wanaamini Akhera. Hao wako juu ya ongofu utokao kwa Mola wao na hao ndio waongufu}} [Al-Baqara : 1 - 5]
Kutekeleza ahadi na kusubiri wakati wa raha au shida. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال تعالى) : وَلَكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آَمَنَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآَخِرِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ وَآَتَى الْمَالَ عَلَى حُبِّهِ ذَوِي الْقُرْبَى وَالْيَتَامَى وَالْمَسَاكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ وَالسَّائِلِينَ وَفِي الرِّقَابِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآَتَى الزَّكَاةَ وَالْمُوفُونَ بِعَهْدِهِمْ إِذَا عَاهَدُوا وَالصَّابِرِينَ فِي الْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ وَحِينَ الْبَأْسِ أُولَئِكَ الَّذِينَ صَدَقُوا وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ )[البقرة: 177]
].
{{Bali wema ni wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Mitume na wanawapa mali – juu ya kuwa wanayapenda- jamaa na mayatima na maskini na wasafiri na waombao na kuwakomboa watumwa na wanasimamisha swala na kutoa zaka, na watekelezao ahadi zao wanapoahidi, na wavumiliao katika shida na raha na wakati wa vita}} [AL-Baqarah : 177].
Kuomba msamaha kwa madhambi yao. Kama Alivyosema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال تعالى) : وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنْفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَنْ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَى مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ )[آل عمران: 135]
{{Na wale ambao wanapofanya uchafu au kudhulumu nafsi zao hukumbuka Mwenyezi Mungu na kuomba msamaha kwa dhambi zao}} [Al-Imraan : 135].
Fadhila Za Taqwa:-
Taqwa hufungua moyo. Kama Alivyosema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال تعالى: (وَاتَّقُوا اللَّهَ وَيُعَلِّمُكُمُ اللَّهُ ) [البقرة: 282]
{{Muogopeni Mwenyezi Mungu atawafundisha nyinyi}} [Al-Baqarah : 282]. Amesema Mola (Subhaanahu wa Taala):
قال تعالى) : (يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا إِنْ تَتَّقُوا اللَّهَ يَجْعَلْ لَكُمْ فُرْقَانًا وَيُكَفِّرْ عَنْكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ وَاللَّهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ )[الأنفال: 29]
{{Enyi mlioamini mkimuogopa Mwenyezi Mungu atawapa ufafanuzi kufafanua baina ya haki na batili na atakufutieni makosa yenu,na kukusameheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa kabisa}} [Anfal : 29]..
Kupata kabuli. Amesema Mola (Subhaanahu wa Taala):
وقال تعالى): (وَيُنَجِّي اللَّهُ الَّذِينَ اتَّقَوْا بِمَفَازَتِهِمْ لَا يَمَسُّهُمُ السُّوءُ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ )
[الزمر: 61] {{Na Mwenyezi Mungu Atawaokowa wale wamchao kwa ajili ya kufaulu kwao hawataguswa na ubaya na wala hatahuzunika}} [Azumar : 61].
Kuokoka na moto na kufaulu kwa nyumba ya furaha. Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala):
)تِلْكَ الْجَنَّةُ الَّتِي نُورِثُ مِنْ عِبَادِنَا مَنْ كَانَ تَقِيًّا )[مريم: 63]
{{Hiyo nidiyo pepo tutakayowarithisha katika waja Wetu wale ambao ni wachaji Mungu}} [Maryam : 63]. Mwenyezi Mungu Atujaalie katika wale wanao muogopa Mwenyezi Mungu nakupata msamaha wake Allah. Muombeni msamaha Yeye peke yake. Hakika Yeye ndie Mwenye kusamehe waja wake wote.
Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu peke yake. Na nashuhudia hakuna anaye pasa kuabudiwa kwa haki ila Yeye, na nashuhudia ya kuwa Muhammad ni mja wake na ni Mume wake. Na Rehma na Amani zimfikie Mtume aliefikisha ujumbe na Akatekeleza Amana na Jamaa zake na Sahaba zake wote
Thawabu za Wanaomcha Mwenyezi Mungu.
Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wale wanaomcha. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
(إِنَّ اللَّهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوْا وَالَّذِينَ هُمْ مُحْسِنُونَ 128)[النحل: 128]
{{Kwahakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanaomcha na wale wafanyao wema}}.
Kufunguliwa Baraka zitokazo mbinguni. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
وقال) : وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَى آَمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِمْ بَرَكَاتٍ مِنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ وَلَكِنْ كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ )[الأعراف: 96]
{{Na lau kama watu wa miji wangaliamini na kuogopa, kwa yakini tungaliwafungulia baraka za mbinguni na radhi. Lakini walikadhibisha tukawapatiliza kwa sababu ya yale waliokuwa wakiyachuma}} [Al-A’raaf : 96]. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
وقال : (وَمَنْ يَتَّقِ اللَّهَ يَجْعَلْ لَهُ مَخْرَجًا )[الطلاق: 2]
{{Na yoyote anaemcha Mungu, Humjaalia matokeo na kumtengenezea njia ya kuokoka na balaa}}.
Ndugu Waislamu na wausia kumcha Mungu ambae ndie anaekuokoa wewe katika siri yako na anakuchunga wewe katika dhahiri yako. Mjaalie Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) moyoni mwako na kwa kila hali; mchana na usiku. Enyi watukufu Waislamu chukueni zawadi za uchaji Mung, bora ya zawadi ni kumcha mungu. Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala):
قال (وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَى( [البقرة: 197]
{{Chukueni zawadi hakika zawadi bora ni kumcha Mungu}} [Al-Baqarah : 196].
Enyi mlioamini mcheni Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala): na iyangalie nafsi imetanguliza nini. Na muogopeni Mungu hakika Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) ni mjuzi kwa mnayoyatenda. Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala):
وقال) وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ نَسُوا اللَّهَ فَأَنْسَاهُمْ أَنْفُسَهُمْ أُولَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ) [الحشر: 19]
{{Na wala msiwe kama wale waliomsahau Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu akawasahaulisha nafsi zao. Hao ndio maasi wakubwa}} [Al-Hashr : 19].
Mwisho:
Ndugu Waislamu na wausia kumcha Mungu Ambae ndie Anaye kuokoa wewe katika siri yako na anakuchunga wewe katika dhahiri yako. Mjaalie Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) moyoni mwako kwa kila hali; mchana na usiku. kumesemwa: Enyi watukufu Waislamu chukueni zawadi za uchaji Mungu na bora wa zawadi ni kumcha mungu. Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Atujaalie katika wanaomcha yeye, Atuhifadhi na machafu, Atupe mwisho mwema tukiondoka duniani.