UHIMIZAJI WA KUSEMA UKWELI NA UTAHADHARISHAJI WAKUSEMA URONGO


3076
wasifu
uislamu ni dini ya ukweli,na umeamrisha waislamu wawe wa kweli,na katika sifa za waumini ni wale wanao sema ukweli,na ukweli humpeleka mtu peponi,na urongo humpeleka mtu motoni,na sifa ya urongo ni sifa ya wanafiki,kwani miongoni za alama ya mnafiki ni kusema urongo.kwa hivyo tumetahadharishwa sana kuwa mbali na sifa kama hiyo.

Asili ya mwanadamu kuwa muovu katika zama zetu inatokana na kuacha dini kubwa nao ni ukweli waja wa Mwenyezi Mungu na kuusieni pamoja na kuusia nafsi yangu juu ya kumcha Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala): “Enyi mlioamini, Mcheni Mwenyezi Mungu na kuweni pamoja na wakweli”. Kuwa na ukweli na Mwenyezi Mungu ndio inaleta imani ya sawa, mkweli huwa anamtegemea Mwenyezi Mungu anasubiri anapopatwa na msiba, anashukuru anapopata neema, anakuwa mzuri kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na anakuwa mbaya pia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwa ajili hiyo amewaamrisha waumini kuwa wakweli, akasema Mwenyezi Mungu:

Uhakika wa ukweli ni pale inapodhihiri katika jamii, na mpaka kuwa na imani kati yao, ienee kati yao heshima na mapenzi, amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Wenye kuuziana wana khiari madamu hawajatengana, wakiwa wakweli hubarikiwa na wakiwa waongo huondolewa Baraka].

Ukweli katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu

Ametaja Mwenyezi Mungu ukweli katika Qur’an tukufu katika Aya nyingi miongoni mwa Aya hizo ni:- Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قوله تعالى: (يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ) [التوبة: 119]

{{Enyi mlioamini, Mcheni Mwenyezi Mungu nakuweni pamoja na wakweli}}. Maamrisho haya ya Allah kwa Waislamu ni wawe wakweli kwa hali yao yote, kwa maneno na vitendo. Na Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

وقوله تعالى: (لِيَجْزِيَ اللَّهُ الصَّادِقِينَ بِصِدْقِهِمْ) [الأحزاب: 24]

{{Ili awalipe wa kweli kwa sababu ya ukweli wao}}. Na neno lake Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

وقال الله تعالى (هَذَا يَوْمُ يَنْفَعُ الصَّادِقِينَ صِدْقُهُمْ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا) [المائدة: 119]

{{Mwenyezi Mungu Atasema: Hii ndiyo siku ambayo ukweli utawafaa ukweli wao}}. Siku ya kiama kitu kitakacho msaidia mwanadamu ni ukweli. Kama alikuwa mkweli duniani basi siku ya kiama ataokoka na Moto wa jahannam.

Aina ya Ukweli

Wanakosea wengi miongoni mwa watu wanapodhani kuwa ukweli ni ule wa maneno pekee, lakini ukweli pia ni wa vitendo na hali. Tunaweza kuweka wazi kama ifuatavyo.

Ukweli wa maneno, inampasa kila mwanadamu kuhifadhi ulimi wake na kutozungumza isipokuwa ukweli, na Mwenyezi Mungu atauliza jambo hilo.

Ukweli wa vitendo ni awe sawa siri yake na dhahiri bila ya kutofautiana kati ya dhahiri yake na usiri wake alikuwa Hassan Basri akiamrisha jambo huwa wa kwanza kulifanya, na akikataza jambo huwa wa kwanza kuliacha. Amesema Mutrif ukiwa sawa usiri wa mja na udhahiri wake, Mwenyezi Mungu husema huu ni mja wangu ni mkweli.

Ukweli katika hali, nao ndio daraja ya juu kuwa mkweli katika ikhlas na kuogopa, toba, kutarajia na nyinginezo.

Uislamu umeheshimu haki ya ukweli, na unachukia uongo na urongo ni alama ya unafiki. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Alama za mtu mnafiki ni tatu: akisema husema uongo, akiahidi huenda kinyume na ahadi yake, akiaminiwa hufanya khiyana”. Ukiangalia hali ya Waislamu leo utaona wana upungufu katika upande wa ukweli, na ndio sababu ya kudhoofika kwa imani, na kuenea kwa maasi, na kupenda dunia. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Ukweli una utulivu na uongo una wasiwasi].

Sura za Uongo:-

Kusema uongo wazazi kuwaambia watoto wao, na uislamu umebainisha kuwa malezi ya watoto yanatakiwa yasipatikane ndani yake uongo, ili wapate kuzoea ukweli. Amepokea ‘Abdallah Bin ‘Amir akisema: “Aliniita mamangu nikiwa mdogo na Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amekaa nyumbani kwetu, akamuuliza mamangu unataka kumpa kitu gani? Akasema: tende, kama hutampa kitu basi utakuwa muongo”

Kuenea uongo katika mazungumzo ya watu, na vitendo vyao.

Amepokea Anas hadithi kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akisema: [Mwenye kuwa na mambo matatu huwa mnafiki, akizungumza husema uongo, akiahidi huenda kinyume, akiaminiwa hufanya khiana].

Kuvunja ahadi, na sura za kuvunja ahadi, kutohudhuria sehemu bila ya sababu, kuchelewa kufika kwa wakati wake.

Kuhini amana, watu wengi hawafanyi wajibu wao kwa namna inavyotakiwa kama kuchelewa kazini na akija mapema utamuona anajishughulisha na simu, kusoma gazeti, kuchukua likizo ya ugonjwa na si mgonjwa.

Kufanya khiana katika mauzo, kama kuficha aibu ya bidhaa na kununuliwa bidhaa yake kwa bei mzuri.

Kutaka kitu na kudai umasikini. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Mwenye kuomba watu ili apate kuzidisha mali yake basi anaomba kaa la moto].

Kuficha mwenye kuposa au kuposwa kwa aibu aliokuwa nao na kudhihirisha uzuri.

Wanaosema uongo mwingi leo ni wafanya biashara, ili kula mali ya watu kwa dhulma. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Madhambi makubwa ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, kuwaasi wazazi wawili, kuua nafsi na kuapa kiapo cha uongo].

Mcheni Mwenyezi Mungu na kumbukeni neno lake Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): “Wakisema ukweli hubarikiwa katika biashara yao, na wakificha na kusema uongo huondolewa baraka” na lau kama wafanya biashara watasema ukweli watabarikiwa katika biashara yao.

Faida ya Ukweli:-

Kuingia peponi, ameulizwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amali ya peponi akasema ni Ukweli na hakuna kitakachomuokoa mwanadamu siku ya kiyama isipokuwa ni ukweli.

Kuafikiwa kwa kila jambo la kheri. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) kumuambia Ka’ab siku ya vita vya tabuuk: [Huyu amesema ukweli].

Kusalimika kutokana na maangamivu, kisa cha watu watatu walio funikwa na pango, mmoja wao akasema: “Haitokuokoeni isipokuwa ukweli, aombe kila mmoja wenu kwa jambo ambalo alilokuwa nalo ukweli”

Kuwa mzuri ndani yake.

Ukweli unaleta maslahi ya duniani na kesho akhera,

Ukweli unaleta utulivu.

Mkweli hadhuriwi na fitna.

Ukweli ndio asili ya wema, na uongo ndio asili ya uovu, kama alivyosema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Jilazimisheni na ukweli kwani ukweli unaleta wema, na hatowacha mtu kusema ukweli mpaka ataandikiwa kuwa yeye ni mkweli, na tahadhari na uongo kwani uongo unaleta uovu, na uovu unapeleka mtu kuingia motoni, na hatoacha mtu kusema uongo mpaka ataandikwa kuwa muongo].

Mkweli hawi mnafiki amesema Mtume Mwenyezi Mungu: [Mnafiki akizungumza husema uongo, akiaminiwa hufanya khiyana, akiahidi hatimizi].

Mkweli huruzukiwa firasa (kuona mbali).

Mkweli husifiwa na sifa nzuri, kama alivyowasifu Mwenyezi Mungu manabii wake

Ukweli huleta Baraka katika mauzo.

Tumuombe Mwenyezi Mungu atujalie ni miongoni mwa waja wake wa kweli na wenye kufaulu siku ya kiama kwa kuingia peponi.

Mwisho

Ndugu Waumini, tumeona wazi umuhimu wa ukweli na kusema ukweli katika mafundisho ya dini yetu. Ukiwa mkweli utapendwa na Mwenyezi Mungu na utapendwa na watu wote. Ukweli ndio ufunguo wa mambo yote ya kheri. Na uongo ni ufunguo wa mambo yote ya shari. Mwenyezi Mungu atuepushe na uongo, na atuafikie kushikamana na ukweli mpaka tuondoke duniani tukiwa wakweli na tukutane na yeye tukiwa wa kweli.





Vitambulisho:




Maisha Mazuri