UKATINAKATI KATIKA QUR’ANI NA SUNNA


3999
wasifu
Uislami ni Dini ya ukatinakati, ni Dini ya uadilifu na msimamo uliyonyoka. Na katika Qur'ani tukufu na Sunna ya Mtume kuna aya na Hadithi nyingi zenye kuonesha ukatinakati wa Uislamu na usawa wake: ukatinakati ambao haunA kwenda kombo, kwa kuwa ni haki iliyoteremka kutoka mbinguni, hakuna kupita kiasi wala kupunguza, haina kuengeza wala kupunguza, haina kukaa ukingoni(siasa kali) wala kutupa na kuacha, haina kudharau wala kuachilia.

Makusudio ya Ukati na kati ni mfumo na njia ya kufuata Qur’an na Sunna za Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) bila ya kuzidisha au kupunguza. Na huo ndio mfumo wa Mtume na Masahaba zake na watu wema walio tangulia. Dini ya Kiislamu imekamilika, hakuna mtu ambae atakuja baada ya Mtume na kudai ana mambo ya ziada katika dini. Na vile vile, hakuna mtu ambae atadai ya upungufu wa Dini. Njia zote mbili hazikubaliki, kwasababu, Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Amesema:

وقال تعالى) الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا)

[المائدة: 3] {{Leo nimekukamilisheni dini yenu, na kuktimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe Dini yenu}}.

Na Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

وقال تعالى(إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ )[الحجر: 9]

{{Hakika Sisi ndio tulioteremsha Qur’an, na hakika Sisi ndio tutakayoilinda}}. Kwa hivyo, Mfumo na Manhaj ya dini ya Kiislamu ni moja nayo ni kufuata Qur’an na Sunna bila ya ziada wala kupunguza.

Ukati na Kati katika Qur’an

Maelezo ya neno lake Allah (Subhaanahu wa Taala) Aliposema:

قال الله تعالى): وَكَذَلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا) [البقرة: 143] {{Tumewafanya (nyinyi Waislamu) kuwa ni umma bora ili muwe ni mashahidi kwa watu (wafuasi wa mitume iliyotangulia kuwa mitume yao waliufikisha kwao ujumbe wa Allah}}.

Kwa sababu Allah amewaeleza vizuri katika Qu’rani Aliposema (Subhaanahu wa Taala).

قال تعالى) كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَر)

[آل عمران: 110] {{Nyinyi ni umma bora uliotolewa miongoni mwa watu, mnaamrisha mambo mema na kukataza mabaya}}..

Ulinganizi wa Mitume wote ulikuwa Mfumo wake na Wakati Na kati

Ushahidi wake ni neno la Mtume lililopokewa kwa Abu Huraira amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) [Hakika dini ni nyepesi wala mtu hatoifanyia dini mkazo isipokuwa itamshinda fanyeni usawa na karibisheni na mubashirie mazuri].

Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala):

قال الله تعالى): قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ) [الأنعام: 162]

{{Sema, hapana shaka swala yangu na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu (zote) ni kwa Mwenyezi Mungu ambaye ni muumba wa walimwengu}}.

Enyi Waislamu, Hapana shaka Mwenyezi Mungu anawaamrisha kati ya watu kuhukumu kwa uadilifu. Hapana shaka Allah anawapa mawaidha mazuri, hapana shaka Allah ni mwenye kusikia, kuona.

Na amesema Allah (Subhaanahu wa Taala):

قال الله تعالى: (وَابْتَغِ فِيمَا آَتَاكَ اللَّهُ الدَّارَ الْآَخِرَةَ وَلَا تَنْسَ نَصِيبَكَ مِنَ الدُّنْيَا وَأَحْسِنْ كَمَا أَحْسَنَ اللَّهُ إِلَيْكَ وَلَا تَبْغِ الْفَسَادَ فِي الْأَرْضِ إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ) [القصص: 77]

{{Na yote (mali) miongoni mwa aliyokupa Mwenyezi Mungu kwa kuitaka nyumba ya Akhera (Kwa kufanya mema na kutoa sadaka). Na wala usilisahau fungu lako la Dunia (kwa starehe). Na fanya wema (kwa waja wa Mwenyezi Mungu. Na wala (kwa sababu ya mali yako) usifanye uchafu katika ardhi. Hapana shaka Allah hawapendi wenye hufanya uchafu}}.

Ukati na kati wa Ahlu Sunnah wal Jamaah katika Itikadi na Kufuata Twaa

Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى): يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ وَلَا تَقُولُوا عَلَى اللَّهِ إِلَّا الْحَقَّ إِنَّمَا الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ رَسُولُ اللَّهِ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَى مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِنْهُ فَآَمِنُوا بِاللَّهِ وَرُسُلِهِ وَلَا تَقُولُوا ثَلَاثَةٌ انْتَهُوا خَيْرًا لَكُمْ إِنَّمَا اللَّهُ إِلَهٌ وَاحِدٌ سُبْحَانَهُ أَنْ يَكُونَ لَهُ وَلَدٌ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَكَفَى بِاللَّهِ وَكِيلًا) [النساء: 171]

{{Enyi watu wa vitabu! msipite mipaka katika dini yenu (hawa ni wakristo wanaodai uungu wa nabi Issa na wala usiseme juu ya Mwenyezi Mungu (kwamba ana mke na watoto) ila mseme haki. Hapana shaka masihi Issa mtoto wa Maryam ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na neno lake alimpelekea Maryam na roho itokayo kwake. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na muamini Mitume yake. Wanaamrishwa wakristo wanaoamini mitume ya Mwenyezi Mungu na miongoni mwao wamuamini Mtume Muhammad (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) na wala msiseme mungu ni nafsi tatu komeni bora kwenu. Hapana shaka Mwenyezi Mungu ni Mungu moja (hana ushirika) ametakasika kuwa ana watoto. Ni vyake vyote vilivyomo ndani ya ardhi na hakika hutosha kuutegemea Mwenyezi Mungu}}.

Kutoka kwa Anas Ibn Malik alisema: ‘Walikuja watu watatu mpaka kwa nyumba za wakeze Mtume wakauliza namna ya ibada za Bwana Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Walipoambiwa walisema sisi tuko wapi na Mtume na yeye amekwisha samehewa madhambi yake yaliyotangulia na yatakayo kuja. Akasema mmoja wao ama mimi nitaswali usiku siku zote. Na mwingine akasema mimi nitafunga siku zote na na sitoacha kufunga na akasema mwingine na mimi nitajiepusha na wanawake sitooa kabisa. Mtume akawajia akawambia: [ Nyinyi ndio mliosema kadha wa kadha naapa kwa Allah mimi ni mnyenyekevu mno kwa Allah kuliko nyinyi na mimi numuogopa Allah kuliko nyinyi lakini nafunga na siku nyingine sifungi na naswali usiku na siku nyingine nalala na mimi huoa wanawake basi mwenye kuacha mwenendo wangu si miongoni mwa watu wangu].

Maneno ya Wanavyuoni Kuthibitisha Ukati na kati wa Ahlu Sunnah

Amesema ibn Jarir At-Twabary na amepokea ya kwamba Allah (Subhaanahu wa Taala) Amewasifu ya kwamba wao ni watu wakati na kati, kwa ajili ya ukati na kati wao katika dini hawakupita mpaka katika dini. Kama walivyofanya wakristo ambao wamepita mipaka katika (tarhib) na wakasema kuhusu nabi issa ambaye nabii issa hakuyasema wala wao si watu (watakasirika) na kama (taksira) ya mayahudi ambao wamebadilisha kitabu cha Allah na wameuwa Mitume yao na wakamsingizia uongo mola wao (Waislamu) ni watu wa kati na kati na wamelingana katika hilo, wakasifu Allah kwa hilo, likawa jambo linalo pendeza zaidi kwa Allah ni lililo kati na kati. Amesema Shatwiby. ‘Ukiangalia katika kitendo cha sheria na ukazingatia utapata ndani yake kuna ukati na kati, na ukipata umelemea sehemu katika sehemu zake hilo ni kutoka na kukabiliana na ile hali ilivyo au ni kutokea katika sehemu nyingine. Sehemu (upande) uliomgumu sana ni kwa kulihofisha na kuhimiza na kukataza. Na upande au sehemu yenye ukhafifu sana inakuwa katika kutoa ruhusa na kuhimiza inakuwa mara nyingi ni uzito kulifanya jambo kuwa gumu, isipokuwa hivi au vile utaona Na upande wa usawa uko wazi nao ni msingi ambao wenye kurejelewa na mwenye akili ni yule ambaye atauelekea”.

Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala) katika Qur’an tukufu kueleza ukati na kati :

قال الله تعالى): كَانَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً فَبَعَثَ اللَّهُ النَّبِيِّينَ مُبَشِّرِينَ وَمُنْذِرِينَ وَأَنْزَلَ مَعَهُمُ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِيَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ فِيمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ وَمَا اخْتَلَفَ فِيهِ إِلَّا الَّذِينَ أُوتُوهُ مِنْ بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ فَهَدَى اللَّهُ الَّذِينَ آَمَنُوا لِمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِهِ وَاللَّهُ يَهْدِي مَنْ يَشَاءُ إِلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ )[البقرة: 213] {{Walikuwa watu ni umma mmoja (juu ya imani mmoja) (wakakhitilafiana) na akapeleka Mwenyezi Mungu Manabii wenye kutoa habari njema (kuwa wenye kuamini kuwa wataingia peponi) na kutoa onyo (kuwa wakafiri kutamba wataingia motoni) na aliwateremshia vitabu vilivyoshikamana kwa haki ili ahukumu kati ya watu katika waliokhtalifiana na hawakukhitlifiana katika vitabu ila walio pewa (hivyo vitabu) baada ya kuwajia wao hoja zilizo waziwazi kwa ajili ya wivu baina yao (uvivu wa makafiri juu ya wenye kuamini) na akawaongoza Mwenyezi Mungu walioamini kwa walivyokhitalifiana nayo katika haki kwa ruhusa yake) na Mwenyezi Mungu humwongoza amtakaye katika Uislamu}}.

Kutoka kwa ibn ‘Abbas amesema: Aliulizwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) ni dini gani inayopendeza zaidi kwa Allah? akasema; [ Al-Hanafiyat Samhaa] Amepokea Ahmad katika musnad. Maana yake ni dini ya kusimamisha Tawhidi ya Allah peke yake na kufuata mila ya baba yetu Ibrahim na kutoka kwa Anas Ibn Malik kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [Fanyeni wepesi na mutoe biashara wala musifukuze watu hakika mimi nimetumilizwa kufanya wepesi].

Na kutoka kwa Abu Huraira amesema: Hakika Bedui alikojoa katika Msikiti watu wakampigia kelele. Mtume wa Allah akawaambia: [Mwacheni, kisha mwagieni maji].

Mwisho

Enyi Waislamu, Hakuna njia nzuri kuliko ile aliyofundisha Mtume na Masahaba zake baada yake na waja wema. Kwa hivyo, tufanyeni bidii kujilazimisha na manhaj ya Mtume sahihi bila ya kuangalia njia nyinginezo ambazo ni ziada ya manhaj ya Mtume au ni upungufu ukilinganisha na Manhaj ya Mtume na Masahaba zake. Ndugu katika imani, Mcheni Allah na jilazimisheni na Kitabu chake na Sunna za Mtume wake.

Tunamuomba Allah Atujalie miongoni mwa waliopata tawfiq yake ya kuweza kufuata Kitabu chake na Sunna za Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam).





Vitambulisho: