UMUHIMU WA KUAMRISHA MEMA NA KUKATAZA MAOVU


3386
wasifu
Kuamrisha mema na kukataza maovu ni jambo kubwa ambalo watu wengi wameghafilika nalo. Ni ubaya uilioje kwa mtu na jamii wenye mwisho mbaya pale wanapojiepusha watafutaji elimu na mabarobaro wazuri kushiriki katika jamii kwenye nyanja zote, na kuacha kufuata njia ya kutengenea kwa kuamrisha mema na kukataza mabaya!

Waja wameumbwa kwa ajili ya ibada, lakini iblisi amewaghuri waja wa Mwenyezi Mungu kwa kutofanya ibada (Swala, Swaum na zenginezo). Dini ya Mwenyezi Mungu ni kufanya maamrisho ya Mwenyezi Mungu, na mwenye kuacha haki za Mwenyezi Mungu basi atakuwa muovu kuliko mwenye kufanya maasi.

Tumewaachia mujtamaa watu waovu, na sisi tumekaa tukitoa aibu zama zetu lakini aibu ziko kwetu. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) : وَلْتَكُنْ مِنْكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ) [آل عمران: 104]

{{Na wawepo katika nyinyi watu wanaolingania kheri, na wanaoamrisha mema na wakakataza maovu. Na hao ndio walio faulu}}.

Na Akasema tena Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) : كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ( [آل عمران: 110]

{{Nyinyi ndio umma bora kuliko umma zote zilizodhihirishwa watu, mnaamrisha yaliyo mema na mnakataza yaliyo maovu na mnamwamini Mwenyezi Mungu}} Amesema Ibn Qayyim: ‘Dini gani na kheri gani kwa mwenye kuona maasi yanafanywa, na mipaka ya Mwenyezi Mungu yanakiukwa na dini yake Mwenyezi Mungu na Sunna zake Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) zinaachwa, na moyo wake kuwa baridi na akinyamaza huyo ni shetani kiziwi, kama mwenye kuzungumza baatil huyu ni shetani anayezungumza na balaa ya dini hii ni kwa wale wanaopewa madaraka na kutojali jambo la dini’.

Ndugu yangu Muislamu una majukumu ya maovu yoyote yale na uweke mikakati ya kutengeneza jamii. Asili ya kuamrisha mema na kukataza maovu ni kwa uharaka, na umuhimu wa kuamrisha mema na kukataza maovu ni kuhifadhika umma kuangamia, na kumakinika katika ardhi hii, amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) : الَّذِينَ إِنْ مَكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ أَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآَتَوُا الزَّكَاةَ وَأَمَرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَوْا عَنِ الْمُنْكَرِ وَلِلَّهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ) [الحج: 41]

{{Wale ambao tukiwamakinisha katika ardhi husimamisha sala na wakatoa zaka na wakaamrisha yaliyo mema na wakakataza yaliyo mabaya}}.

Na mwisho mbaya ni pale wanafunzi wa dini na mabarobaro wanapo jishughulisha na mambo mengine na kuwacha kutengeneza jamii, na kutoamrisha mema na kukataza maovu. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Mtaamrisha mema au mtakataza maovu, au nahofia itawateremkia adhabu, mumuombe Mwenyezi Mungu na asiwakubalie dua zenu]. Imepokewa na Zainab akisema “Je tutaangamia na kuwa watu wema? Akasema ndio ukizidi uchafu”.

Na Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) : لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَى لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ذَلِكَ بِمَا عَصَوْا وَكَانُوا يَعْتَدُونَ كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَنْ مُنْكَرٍ فَعَلُوهُ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ) [المائدة: 79]

{{Walilaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa Israil kwa ulimi wa Dawud na wa ‘Isa bin Maryam. Hayo ni kwa sababu waliasi na wakapindukia mipaka. Hawakuwa wenye kuzuiana mabaya waliyokuwa wakiyafanya. Uovo ulioje wa jambo hili waliokuwa wakilifanya}}.

Uovu ambao unapaswa kuzuiwa ni:

Uwe umekatazwa kisheria.

Uwe unafanyika sasa.

Uwe dhahiri uovu huo.

Usiwe uovu ni katika masuala ambayo wamehitilafiana wanazuoni.

Amesema Sheikh Ghazal, anayefanya maasi adhabu yake kuna aina tatu:-

Kuwa nzito na ngumu, hii inakuwa kwa anayefanya makosa ya hudud na taaziri, hii ni kwa wenye majukumu.

Kuwe maasi hayo inawezekana kufanyika kama kuvaa hariri kuzuia maasi hayo ni wajibu.

Uwe uovu huo unawezekana kufanyika kama yule anayefurahika kufagia sehemu ya tembo, mtu kama huyu anafaa kupewa mawaidha, ama kupigwa haifai isipokuwa akijua sehemu siku zote ni ya kunywa tembo.

Kuweka wazi masharti manne yaliyotangulia:

Uwe ni uovu (munkar) mfano ukimuona mtoto mdogo au mwendawazimu anakunywa tembo inapaswa kuimwaga tembo (pombe) hilo na kumzuia, vile vile ukimuona mwendawazimu anazini na mwendawazimu mwenzake inapaswa kumzuia.

Uwe uovu huo unafanyika, kwa sasa pia kula atakayejua kwa makadirio kuwa uovu utafanyika, au mwenye kuazimia kunywa tembo (pombe) usiku, kwa huyu mtu wa mwisho inapaswa kupewa mawaidha.

Uwe uovu huo uko wazi bila ya kuchunguza, kwa hiyo kila atakayefanya maasi kwa kujificha na kufunga mlango wake haifai kumchunguza, kisa cha ‘Umar bin Khattab aliporuka ukuta wa mtu mmoja na kumuona katika hali ya kuchukiza akamkataza ‘Umar. Yule bwana alimuambia ‘Umar kuwa yeye amemuasi Mwenyezi Mungu kwa njia tatu:- kuchunguza, kuingia kwenye nyumba pasipo na mlango wake na kuruka ukuta, ‘Umar akamuacha na akamshurutisha kutubia kwa Mwenyezi Mungu. Kwa ajili hiyo haifai kuingia katika nyumba mpaka idhihirike kama kusikia sauti au herufu ya tembo (pombe), hapo ndipo unaruhusiwa kuingia na kuzuia munkar. Na kudhihirika kwa kitu ima ni kwa kusikia, kuniusa, kuona, kushika.

Uwe unajulikana munkar huo bila ya kujitahidi kuwa inafaa au haifai. Haifai kwa Hanafy kuwakataza Shafy Bismillah wala haifai Shafy kuwazuia Hanafy kwa kunywa (wabidh) aina ya tembo, kutokana na kuhitalifiana wanazuoni kwa masuala yaliyo magumu, wamesema baadhi ya wanazuoni haifai kuzuia uovu ila kwa mambo yaliyo haramu.

Amepokea Abi Said Khudhriy hadithi kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akisema: [Mwenye kuona uovu basi auzuie kwa mkono wake, na asipoweza basi atumie ulimi wake, na asipoweza atumie moyo wake, na huo ni udhaifu wa iman].

Daraja za kuzuia Uovu:-

Mwanzo kutumia mkono,

Kutumia ulimi

Kuchukia, na kama uko hapo inapaswa uondoke.

Adabu za kuzuia Uovu:-

Kujua uovu,

Kusubiri,

Kuwa na ikhlas,

Kuwa mpole,

Kuwa kiigizo chema.

Mwisho

Ndugu Waislamu, kwa hakika jamii haiwezi kusimama juu ya msimamo wa dini mpaka nguzo hii ya kuamrisha mema na kukataza maovu isimamishwe. Leo tunashuhudia katika jamii yetu ya kiislamu maadili na akhalaqi mbaya kwa sababu ya kukosekana nguzo ya kuamrisha mema na kukataza maovu. Ndugu katika imani, ni jukumu la kila Muislamu kubeba hamu ya nguzo hii muhimu kuanzia kwake nyumbani hadi kwa jamii yote.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu asituteremshie laana kama alivyo wateremshia wana wa Israel. Ewe Mwenyezi Mungu usituadhibu kwa makosa wanaofanya wengine. Ewe Mwenyezi Mungu tubariki na utusamehe madhambi yetu.





Vitambulisho:




Aina nyengine za zaaka