Afanye Wudhuu Kila Baada Ya Kunyonyesha?


277

SWALI: Napenda kupata uhakika kuhusu wudhuu kamili mimi ninanyonyesha kwani ni lazima kila ninapotaka kutia wudhu kwa ajili ya swala nisafishe chuchu? Au naweza kunyonyesha nikiwa na wudhu kisha nikaendelea kuswali ama mpaka nikatawadhe tena?

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani zetu za dhati kwa dada yetu kwa swali lako hilo. Hakika ni kuwa kunyonyesha si katika mambo yenye kutengua au kuharibu wudhuu. Hivyo, unapomaliza kunyonyesha na ukawa una wudhuu wako utaweza kwenda kuswali bila kuchukua wudhuu mara ya pili. Na Allaah Anajua zaidi






Vitambulisho:




MISINGI YA UWEKAJI SHERIA