JIBU: Inawajibika kwa mwanamke aliyejifungua katika mwezi wa Ramadhwaan kulipa siku alizokuwa hakuweza kufunga siku za mbele. Na ikiwa hakulipa siku hizo bila sababu inayokubalika katika Shariy’ah ya Kiislamu hadi imeingia Ramadhwaan nyingine, basi inampasa alishe maskini kwa idadi ya siku alizokuwa hakufunga na pia afunge Swawm za siku hizo. Lakini kama kuchelewa kulipa kulikuwa kwa sababu inayokubaliwa katika Shariy’ah ya Kiislamu basi inamtosha kuzilipa tu siku hizo. Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam. [Fataawa Ramadhwaan - Mjalada (2), Ukurasa (588), Fatwa Namba (573); Fataawa Al-Lajnah Ad-Daaimah lil-Buhuwth Al-'Ilmiyyah wal-Iftaa. - Fatwa Namba (9861)]