Amepata Hedhi Baada ya Tendo La Ndoa Kabla ya kuoga Janaba


877

SWALI LA KWANZA Assalamu alaykum warahmatullahi wabarakatuh; Natanguliza shukrani kwa Mola Muumba wa Ulimwengu, Mwingi wa Rehma na Mwenye kurehemu. Sala na Salamu zimfikie Mtume wetu Muhammad Swallah Allahu Alayhi wasallam. Napenda pia kuchukua nafasi hii kuwapa pongezi ndugu zetu kwa kuanzisha na kuendeleza mtandao wenye kheri wa alhidaaya.com . Allah Awalipe kheri fi ddunya wal akhar InshaAllah. Suala langu lipo kama ifuatavyo: Mwanamke aliyefanya tendo la ndoa na kabla ya kufanya ghuslu ya janaba akapatwa na damu ya hedhi. Mwanamke huyu atawajibika kukoga janaba au josho tu la kawaida. Na akitwaharika kutokana na damu ya hedhi, jee atarudia kuoga ghuslu ya janaba kisha aendelee na kukoga hedhi? Assalamu alaykum! SWALI LA PILI LA MUULIZAJI MWENGINE Assalaam aleykum. Mimi nilikua nina swali Kama mwanamke yuko karibu ya kupata siku za hedhi, namaanisha bado hajapata anasubiri wakati wowote inaweza tokea. Na mwnamke huyo akakutana na mume wake pindi anamaliza kitendo cha ndoa na kabla hajaoga janaba ana pata hedi. Sasa anaweza kuoga janaba wakati ana hedi? au inakuwaje wakati janaba imeakutana na hedi namna ya kujitwaharisha ni kama kawaida unaoga janaba, kisha baada ya siku za hedi kwisha unaoga hedi? Insha'alah natarajia Kwa neema za mwenye'ezi mungu kuweza kunijibu swali langu. Shukran

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Kuna rai tofauti za Maulamaa kuhusu mas-ala haya; kuna waliosema kwamba mwanamke aliyetoka kwenye janaba kisha akapata hedhi hana haja ya kuoga ghuslu ya janaba kwa sababu hali yake itakuwa hajatwahirika, hivyo atakapomaliza hedhi atafanya ghuslu kwa nia mbili ya kuondosha janaba na kuondosha hedhi. Ama rai nyingine na ambayo ndiyo bora zaidi na yenye usahihi zaidi , na Allaah Anajua zaidi, ni kwamba mwanamke anapotoka kwenye janaba kisha akapata hedhi afanye ghuslu ya janaba kwanza kisha atakapomaliza hedhi afanye ghuslu ya hedhi. Rai hii zaidi ni ya Maulamaa waliotoa hukumu kwamba mwenye janaba hawezi kusoma Qur-aan, bali mwenye hedhi anaweza kusoma, hivyo kufanya ghuslu kuondoa janaba kutamruhusu mwanamke kupata fursa ya kusoma Qur-aan. Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema katika Al-Mughniy (1/134): "Mwanamke akifanya ghuslu ya janaba wakati amepata hedhi, ghuslu yake itafaa na atatoka katika hukmu ya janaba" Hii ni rai ya Imaam Ahmad pia ambaye amesema: "Mwanamke atatwaharika na Janaba lakini atakuwa bado hajatwaharika na hedhi hadi damu isite". Akasema: "Simjui yeyote aliyesema kwamba mwanamke haimpasi kufanya ghuslu isipokuwa 'Atwaa, hata hivyo imesimuliwa kuwa amesema mwanamke afanye ghuslu" Kwa hiyo ni bora mwanamke aliyefikwa na hali hiyo afanye ghuslu ya janaba kwanza ili kujitoa katika hali hiyo. Na Allaah Anajua zaidi






Vitambulisho:




NJIA YA UTUKUFU