Amesikia Muadhini Wa Alfajiri Hali Akiwa Anakunywa Je, Swawm Imesihi?


263

SWALI: nilikuwa nakula daku nilivo maliza kula nikawa nakunywa maji wakati naendelea kunywa maji nikasikia wanaadhini nikaendelea kunywa maji yaliomo mdomoni, je swaumu yangu imekubalika?au inabidi nilipe?naomba nijibiwe haraka, asanteni saana.

JIBU: AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho. Swawm imesihi ikiwa hali ni kama ulivyotaja kuwa ulisikia Muadhini na huku ulikuwa umeshaanza kunywa maji. Hii ni kutokana na dalili ya usimulizi ufuatao: عن ابن عمر رضي الله عنهما قال: كان لرسول الله صلى الله عليه وسلم مؤذنان بلال وابن أم مكتوم .فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم ((إنَّ بِلاَلاً يُؤَذِّنُ بِلَيْلٍ فَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّى يُنَادِيَ ابنُ أمِّ مَكْتُومٍ) متق عليه Kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ambaye amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na waadhini wawili; Bilaal na Ibn Ummi Makhtuwm akasema: ((Hakika Bilaal anaadhini usiku (adhana ya mwanzo), basi kuleni na mnywe hadi aadhini Ibn Ummi Makhtuwm)) [Al-Bukhaariy na Muslim] Na Allaah Anajua zaidi






Vitambulisho:




Allah Aliye karibu