Amewajibikiwa Zakaah Lakini Pesa Anazopata Anazihitajia Kwa Matibabu Na Kujenga Nyumba


304

SWALI: JE IWAPO NAISHI MAISHA YA KUJINYIMA ILI NIKUSANYE PESA KWA AJILI YA KUJENGA JAPO KIBANDA CHA KUISHI AU NIPATE PESA ZA MATIBABU KISHA IKAPINDUKIA MWAKA. JE NINA WAJIBU WA KUTOA ZAKAAH KWA PESA HIZO?

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani kwa swali lako kuhusu uwajibikaji wa kutoa Zakaah pesa zipitapo mwaka mmoja. Pindi pesa zifikiwapo na mwaka na zikawa ni kiwango cha chini basi ni lazima mwanzo uitolee Zakaah kabla ya kufanya jambo lolote lile. Hilo ni deni la Mwenyezi Mungu, na deni hilo ni muhimu sana kulipwa. Baada ya kulipa Zakaah ifaayo kulipwa waweza kutumia zinazobakia kwa matibabu na kujenga nyumba. Na kwa nini ujitie wasiwasi kwani Zakaah ni kiasi kidogo sana cha fedha; ni 2 ½ % Na Allaah Anajua zaidi






Vitambulisho:




Mahmoud Khaleel Al Hussary - Quran Downloads