Anapoharibu Mimba, Afanye Wudhuu Au Ghuslu?


450

SWALI: Mimi nina swali langu moja je DAMU ya mimba iliotoka au kutolewa ikisha isha mwanamke hujipa udhu vipi samaha ikiwa kama swali litakua limesha ulizwa sana na wengine

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu cha kufanya mwanamke anapoharibu mimba. Katika kuoga josho la janaba ima kwa kukatika kwa damu ya nifasi au damu ya mwezi mwanzo unaanza na kuchukua wudhuu kama wa Swalah. Baada ya hapo unaoga mwili mzima. Hii ndio njia ya kuoga baada ya damu kumalizika. Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi Ghuslu - Vipi Kukoga Janabah, Nifaas Na Hedhi 044 - Kuoga (6) Kuoga Mwanamke Janaba, Hedhi Na Nifaas, Na Kukausha Viungo Baada Ya Kuoga 045 - Kuoga (7) Masuala Yanayohusiana Na Kuoga Na Allaah Anajua zaidi






Vitambulisho:




Kuwa Mbobezi