Du'aa Za Kujitwaharisha


793

SWALI: Ukitia wudhuu na ukasahau kusoma dua inayotakiwa katika kiungo fulani, je, unaweza kurudia kiungo hicho mathan ikiwa hujafika mbali?

JIBU Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Hakuna duáa ya kutawadha kila kiungo katika wudhuu, akifanya mtu hivyo basi atakuwa amefanya bid'aa kwani hayo ya kusoma Duáa yamekuja katika mapokezi dhaifu yasiyotegemeleka. Duáa ni mwanzo tu unasema Bismillah ambayo ni lazima kama ilivyo katika hadithi hii : ((عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال لا وضوء لمن لم يذكر اسم الله تعالى)) رواه أبو داود. ((Imetoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه kwamba amesema Mtume صلى الله عليه وسلم : Hakuna wudhuu kwa asiyetaja jina la Allaah سبحانه وتعالى )) Abu Dawuud Ukishaanza wudhuu basi hakuna tena dua yeyote ila baada ya kumaliza wudhuu ambapo unasoma dua yake ya kupata fadhila za kufunguliwa milango minane ya pepo kama ilivyosema hadithi hii: ((عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ما منكم من أحد يتوضأ فيسبغ الوضوء ثم يقول أشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له وأشهد أن محمداً عبده ورسوله اللهم اجعلني من التوابين واجعلني من المتطهرين إلا فتحت له أبواب الجنة الثمانية يدخل من أيها شاء )) رواه الترمذي ((Imetoka kwa 'Umar رضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم kasema: Hakuna katika mmoja wenu atakayetawadha akautengeneza wudhuu kikamilifu, kisha akasema : (Ash-hadu alla Ilaaha illa Allaah wahdahu laa shariyka LahuWa ash-hadu anna Muhammadan 'abduhu wa Rasuuluhu, Allahumma-j-'alniy minat Tawwabiyn waj'alniy minal-mutatwahiriyn) “Nakiri kwa moyo na kwa kauli kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Allaah peke Yake, wala Hana mshirika wake, na ninakiri kwamba Muhammad صلى الله عليه وسلم ni mja wake na ni Mtume wake” “Ee Allaah nijaalie niwe miongoni mwa wale wanaoomba msamaha, na nijaalie miongoni mwa wale waliosafi" isipokuwa atafunguliwa milango minane ya pepo aingie wowote autakao )) At-Tirmidhiy Zifautazo ni adabu na duáa za kuingia chooni na kutoka pamoja na wudhuu Duáa ya kuingia chooni (Ingia kwa kutanguliza mguu wa kushoto) (بِسْمِ الله ) اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِـكَ مِـنَ الْخُـبْثِ وَالْخَبائِث “(Kwa jina la Allaah ) Ee Allaah najilinda kwako kutokana na mashetani ya kiume na ya kike” Duáa ya kutoka chooni (Unapotoka anza kutanguliza mguu wa kulia) غُفْـرانَك “Nakuomba msamaha (Ee Allaah) Duáa ya kabla kutawadha بِسْمِ الله “Kwa jina la Allaah (nina tawadha) Duáa baada ya kutawadha أَشْهَدُ أَنْ لا إِلَـهَ إِلاّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَريـكَ لَـهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمّـداً عَبْـدُهُ وَرَسـولُـهُ “Nakiri kwa moyo na kwa kauli kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Allaah peke yake, wala Hana mshirika wake, na ninakiri kwamba Muhammad صلى الله عليه وسلم ni mja wake na ni Mtume wake” اللّهُـمَّ اجْعَلنـِي مِنَ التَّـوّابينَ وَاجْعَـلْني مِنَ المتَطَهّـرِينَ “Ee Allaah nijaalie niwe miongoni mwa wale wanaoomba msamaha, na nijaalie ni miongoni mwa wale walio safi “ سُبْحـانَكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمدِك أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلهَ إِلاّ أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيْك “Utakatifu ni Wako, Ee Mola wangu, na shukurani zote zinarudi Kwako, nakiri kwamba hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Wewe, naomba msamaha wako, na narejea kwako (kwa kutubia )” Na Allaah Anajua zaidi






Vitambulisho:




Nguzo za Swala