Ikiwa Katokezea Mtu Kutaka Kuunga Jama’aa Naye Anaswali Swalaah Ya Sunnah Afanyeje?


444

SWALI: Endapo ninasali swala ya Sunnah ya baadiya akaja mtu mwingine nyuma yangu (akaniunga jamaa) jee nimsalishe hali ya kuwa mimi naswali Sunnah ya baadiya? Na kama sivyo nimuonyeshe ishara gani?

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kumswalisha mtu anayeswali faradhi ikiwa wewe unaswali Swalaah ya Sunnah. Inajuzu kwa mwenye kuswali Swalaah ya Sunnah kumswalisha mwenye kuswali Swalaah ya faradhi. Kwa hivyo, ikiwa Muislamu amekuja kukufuata utamswalisha bila ya tatizo lolote lile na nyote Swalaah zenu zitakuwa sawa. Na Allaah Anajua zaidi






Vitambulisho: