Imaam Ibn #039;Uthaymiyn: Kusikiliza Nyimbo Baada Ya Swalaah; Je, Swalaah Itakubaliwa?
323
SWALI:
Baadhi ya nyakati huwa nasikiliza nyimbo baada ya Swalaah. Mfano huenda kuswali kisha nnapoingia garini husikiliza nyimbo. Je Swalaah yangu itakubaliwa?
JIBU:
Ama kuhusu Swalaah yako ni sahihi. Lakini kusikiliza nyimbo ni haramu. Kwa hiyo inakuwajibika kuacha ee ndugu! Bali ni bora kwako usikilize Qur-aan au khabari (redioni) ili uokoke na madhambi haya.
[Fataawa Kuhusu Swalaah]