Imaam Ibn Baaz - Kula Mirungi Na Kuhusiana Na Swalaah


943

SWALI: Wengi katika waraibu wa Mirungi, inapofika wakati wa Swalaah basi (kwa wale wanaoswali) hutoa midomoni mwao (Mirungi) na kisha huitema kwenye mifuko ya plastiki kisha huswali. Na baada ya Swalaah huichukua kutoka kwenye mfuko na kuila tena, je, Mirungi ni najisi? Na nini hukmu ya mtu mwenye kuswali na hali imo kwenye mdomo wake? Na je, inajuzu kwa yule mwenye kuila akachelewesha Swalaah hadi amalize kula, kisha aje kulipa Swalaah zake?

JIBU: Sina elimu ya chenye kuonesha kuwa ni najisi, kwani huo ni mti maarufu, na asli kuhusiana na miti na mimea mbalimbali ni kuwa yote ni twahara. Ama utumiaji wake ni haraam kwa kauli sahihi za Wanachuoni kutokana na madhara yake mengi. Na inawapasa hao wenye kutumia, wasiitumie kabisa wakati wa Swalaah, na wala haijuzu hata kidogo mtu kuchelewesha Swalaah kwa ajili hiyo, bali inampasa Muislam aiswali Swalaah kwa wakati wake katika Jama’aah pamoja na ndugu zake Waislam Misikitini, kwa kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Atakayesikia Wito wa Swalaah (Adhaan) na asiende kuswali, basi hana Swalaah ila kwa udhuru.” (Ibn Maajah, Ad-Daaraqutwniyy na Al-Haakim kwa Isnaad sahihi) Na aliulizwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kuhusiana na huo ‘udhuru’ ambao umeruhusiwa, akajibu: “Ni khofu au maradhi”, na matumizi ya mirungi si udhuru wa ki-shariy’ah, bali ni jambo la munkar, na ikiwa mtu atachelewesha Swalaah kwa sababu hiyo, basi hiyo itakuwa ni dhambi kubwa sana. Na haifai vilevile kuunganisha Swalaah mbili kwa sababu ya mirungi, kwani huo si udhuru wa ki-shariy’ah unaokubalika…” [Fataawa Islaamiyah Juz. 3, uk. 445 – Majmu’ Fataawaa wa Maqalaat Mutanawwi’ah, Juz. 23]






Vitambulisho:




Haifai Kufunga Swawm Ayyamut-Tashriyq (Masiku ya 11-13 Dhul-Hijjah)