Inafaa Kusoma Qur-aan Kwa Kutazama Mus-haf Katika Swalaah Za Sunnah?


1813

SWALI: Assalaam alaykum. My dear brothers. My question is.is it possible to my Sunnah prayers, while reading the suraz by holding the holly Qur'aan in my hand? I did not memorize those suraz, I would like to know if it is possible. Asslm alekum. Niliuliza suali,kusoma qurani katika sala kwa kushika kitabu mkononi kusoma sura,je inakubalika hilo,naomba jibu.tfdhli,kwani mimi sijajua kusom kwa moyo bado. asanteni.

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kufaa kushika msahafu na kusoma kwayo katika Swalah za Sunnah. Hakika ni kuwa inajuzu kwa Muislamu kushika msahafu na kusoma kwayo akiwa anaswali Swalah za Sunnah bila ya tatizo lolote na hasa ikiwa ni Swalah ya usiku (kama Tahajjud) ambayo inahitajika kuwa ndefu kiasi. Na Allaah Anajua zaidi.






Vitambulisho:




Ahmed Naina