Inafaa Kuswali Na Nguo Ya Ndani Ambayo Haina Mkojo, Kinyesi Wala Damu Ila Ni Harufu tu?


430

SWALI: ASALAM ALEHKUM POLENI NA KAZI, NA MWENYEZI MUNGU ATA WAJAALIA NGUVU ZAIDI ILI MUWEZE KUTUSAIDIA SISI. SWALI YANGU KAMA IFUATAVYO. JE KUSWALI NANGUO YA NDANI HAI FAI MWANAMKE KAWAIDA ANAKUA NA HARUFU KIASI SEHEM ZAKE JE KAMA NGUO YAKE IMEPATA JASHO IKATOA HARUFU JE ITA WEZEKANA KUSWALIA (NGUO HIYO INAKUA AINA MKOJO, WA KINYESI WALA DAMU NI HARUFU TU. NITASHUKURU KAMA MTANIJIBU HARAKA. NAWATAKIA KAZI NJEMA

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu kuswali na nguo ya ndani ambayo haina mkojo wala kinyesi lakini ina harufu. Harufu ya jasho haitengui wudhuu wala haifanyi nguo ya ndani au ya nje kuwa najisi. Linalohitajika ni kuwa kwa sababu ya unadhifu wa Muislamu, mwanamke au mwanamme, anapokuwa katika hali hiyo anawaudhi wengine. Kitu anachoweza kufanya ni kujisafisha ili kuondoa hiyo harufu tu. Pia ni vyema Muislamu anaposwali awe na unadhifu kamili kwani anamkabili Mola Mtukufu Anayestahiki kukabiliwa kwa usafi wa kila aina: sehemu ya kuswalia, nguo za kuswalia na mwili wote uwe msafi na wenye manukato mazuri. Na ndio maana ikakatwza katika Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kutokuwa na harufu ya vitunguu mtu anapokwenda kuswali Soma zaidi masuala ya Fiqh ndani ya kiungo hiki: Swahiyh Fiqhus Sunnah Na Allaah Anajua zaidi.






Vitambulisho:




Msikiti…Chuo Kikuu