JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho Hakuna vibaya mtu kuongea na mke wake katika simu na kuzungumza maongezi ya mapenzi kwani huyo ni halali yako, kwa hiyo hakuna tofauti ya kuongea naye kwa simu au unapokuwa naye. Inapofika hali hiyo uliyoitaja ya baada ya mazungumzo na kutokwa na manii japo kuwa hukujimai naye mke wako, inakubidi ufanye Ghuslu na hii ni kutokana na dalili ya Hadiyth ifuatayo, kwamba Ummu Sulaym رضي الله عنها alimuendea Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akamuambia: "إن الله لا يستحي من الحق فهل على المرأة من غسل إذا هي احتلمت" فقال صلى الله عليه وسلم : " نعم إذا هي رأت الماء" “Ee Mtume wa Allaah! Allaah Haoni haya juu ya ukweli. Je, mwanamke inampasa afanye Ghuslu pindi akiota?" (Akiota ndoto ya kujimai) Akasema: ((Ndio, anapoona maji)) (Al-Bukhaariy na Muslim). Kwa kupata maelezo zaidi kuhusu mas-ala haya tafadhali soma jibu la swali katika kiungo kifuatacho: Ikiwa Mtachezeana Tu Na Kutokwa Manii Inapasa Kukoga Josho? Na Allaah Anajua zaidi.