Kachukua Wudhuu Kisha Akaangalia Sinema Za Uchi Na Kusimkwa, Swalah Yake Inakubalika Kwa Wudhuu Huo?


442

SWALI: Assalamu alayka, ama baada ya salamu mimi nikijana wa kiislamu ambae na penda kujifunza juu ya uislamu, Ustadh napenda kuuliza swali kama ifuatavyo, Kuna dhana kua mtu hutengukwa na udhu endapo atamgusa msichana/ mwanamke ambae anafaa kumuowa (na kwa mwanamume ni kama hivyo) kwa lengo la matamanio, sass swali liko hapa, mtu anapochukuwa udhu na baadae akaingia ktk vibanda vya sinema za ngono, akaangalia kiasi cha misuli yake kupata joto ila hakutokwa na chochote, muda wa swala ulivyo fika alitoka na kuelekea msikitini na akaanza kuswali kama wenzake. Je? swala ya mtu huyu inakubalika na mtu huyu udhu wake upo?

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kusimika wakati wa kutazama sinema ya ngono na kisha kuswali bila kuchukua wudhuu mara nyingine. Ama kumgusa mwanamke ni makosa kwa mwanamme kwani Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza hilo na kutuambia kuwa ni bora mtu kupigwa msumari wa chuma kuliko kushika mkono wa mwanamke asiye maharimu wake. Kufanya hivyo ni dhambi japokuwa hakuvunji wudhuu ikiwa amemshika bila matamanio. Ama tukija katika swali lako la pili kuhusu kutazama sinema ya ngono na kusimika katika kutekeleza hilo. Hakika ni kuwa haifai kwa Muislamu – mwanamme na mwanamke kutazama sinema kama hizo na mwenye kutizama anapata dhambi ya kuzini kwani kila kiungo kinazini kama macho na viungo vinginevyo. Na huko pia ni kukaribia zinaa ambayo Allaah Aliyetukuka Ametukataza kufanya hivyo. Anasema Aliyetukuka: “Wala msikaribie uzinzi, kwani huo ni uchafu na njia mbaya kabisa” (al-Israa’ [17]: 32). Ama kusimika (mishipa ya sehemu za siri kusimama) huko hakuvunji wudhuu, kwa hivyo anaweza kuswali bila kuchukua wudhuu kwa mara nyingine. Kwa hiyo, atapata madhambi kwa kutazama sinema ya ngono lakini Swalah yake itakuwa sahihi. Na Allaah Anajua zaidi






Vitambulisho:




Samahani Kidogo