Kuanza Katikati Ya Surah Katika Swalaah Inafaa? Je, Aanze Na BismiLLaah?


325

SWALI:

JIBU: AlhamduliLLaah - Sifa njema zote Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuanza Surah katikati katika Swalah. Hakika inafaa kuanza Surah katikati wakati unaposoma Surah katika Swalah. Na unapoanza katikati huwa hakuna kusoma BismiLlaahi ila ikiwa ni ile BismiLlaahi ambayo ni katika Suratun Naml (27), Aayah ya 30. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisoma katikati ya Surah kama ilivyo katika Swahiyh Muslim, Sunan Abi Daawuud na an-Nasaaiy kuwa alikuwa akisoma Suratul Baqarah [2], Aayah ya 136, au aal-‘Imraan [3], Aayah ya 52 au 64 katika baadhi ya Swalah. Na Allaah Anajua zaidi






Vitambulisho: