Kulipa Fidia Kwa Ajili Ya Swawm


269

SWALI: Ni vipi namna ya kutoa vibaba kwa ajili ya mtu asiyeweza kufunga. Unatoa kiasi chote kinachostahili kwa mara moja au unatoa kila siku moja na kiasi chake?

JIBU: Shukrani kwa dada yetu ambaye ameuliza maswali haya ambayo ni muhimu sana kueleweka vilivyo miongoni mwetu. Na majibu yake ni kama yafuatayo: Fidia kwa mtu asiyeweza kufunga wakati wa Ramadhan wala kulipa baada ya Ramadhwaan. Ikiwa mtu ni mgonjwa mtu na anatarajiwa kuwa atapona na hivyo kuweza kufunga itabidi anapokuwa mzima alipe siku alizokula. Lakini ikiwa ni mkongwe au ana ugonjwa asiotarajia kuwa atapata sahali basi itabidi atoe vibaba viwili (nusu pishi) kwa kila siku aliyokula. Allaah anasema: “Na wale wasioweza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini” [Al-Baqarah: 184]. Aayah hii inatueleza kutoa fidia kwa kutoweza kulipa siku ulizokula kwa kumlisha masikini mmoja kwa kila siku. Hapa unaweza ima ukamwalika masikini aje ale nanyi kwa mwezi mzima wa Ramadhwaan au pia unaweza kuwaalika masikini sawa na idadi ambayo hukufunga. Fidia ni nusu swaa' (pishi) ambayo ni sawa na vibaba viwili; navyo ni sawa na kilo moja na nusu (1.5kg). Ikiwa unataka kumpatia chakula unaweza kuchagua kima ambacho unaweza kumpatia masikini au ukakisia mwenyewe chakula cha masikini mmoja kwa siku moja. Kwa mfano ikiwa ni mchele, ngano, tende au chakula maarufu kinacholiwa hapo mnapoishi utatoa kiasi cha kilo moja nusu kwa maskini mmoja. Na Allaah Anajua zaidi






Vitambulisho:




Tabia za Utume.