Kuna Du'aa Khaswa Baada Ya Kumaliza Nifaas (Damu Ya Uzazi) ?


402

BAADA YA KUJIFUNGUA KWA MWANAMKE NA KUKAA SIKU 40 JE DUA YAKE NI IPI? ILI NIWEZE KUENDELEA NA IBADA

BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu wa Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa ‘Aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa Ba’ad, Mwanamke anapotoka kujifungua uzazi huwa katika hali ya 'nifaas' (kutokwa damu ya uzazi). Na hali hii huwa inategemea kila mtu alivyojaaliwa kuwa nayo. Baadhi ya wanawake huwa katika hali hiyo kwa muda wa siku arubaini, wengine zaidi ya siku arubaini, wengine chini ya siku arubaini. Anapomaliza tu mwanamke kutokwa na damu ya nifaas basi anatakiwa aendelee na ibada yake ya kuswali na kufunga kama kawaida hata kama hakuchukuwa siku nyingi kuwa katika hali ya nifaas. Mfano hata kama alikuwa na damu ya nifaas kwa wiki mbili tu, basi pindi atakaposita damu na kuona maji meupe ya kutoharika atakuwa amemaliza nifaas na aendelee kufanya ibada yake kama kawaida, na kutimiza mengine yote kama kawaida. Tutambue kuwa hakuna nasw yoyote katika Qur-aan au Sunnah iliyotaja idadi ya siku za nifaas kwa mwanamke, ila tu imetajwa hivyo kuwa ni taqriban wengi wa wanawake huwa katika hali ya nifaas kwa muda huo au zaidi ya muda huo kwa siku chache au chini ya muda huo kwa siku chache, ndio ikawa imechukuliwa kiasi ya siku arubaini. Na kurudia katika ibada baada ya nifaas hakuna du'aa yoyote iliyo makhsusi katika mafundisho ya Sunnah, bali ni kukoga josho kama josho la hedhi au janaba, kwa kuweka niya moyoni (Na sio kutajwa mdomoni), na kuendelea na Swalah yake. Na Allaah Anajua zaidi






Vitambulisho:




Tafsiri ya quran in swahili SURAT AL- A'RAAF