JIBU: AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho. Hakuna Du’aa maalumu katika Swalaah hii, bali unaweza kuomba baada ya kuimaliza Du’aa zozote upendazo mwenyewe. Bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi kuhusu Swalaah hiyo: Swalah Ya Dhwuhaa - Rakaa Zake, Fadhila Zake na Wakati Wake Na Allaah Anajua zaidi