Kupaka Maji Shingoni Wakati wa Kuchukua Wudhuu Imo Katika Hadiyth?


362

SWALI: Assalam Aalaykum Warahamatullah Wabarakatuh. Ningependa kufahamu jee kuna Hadiyth yoyote kua Bwana Mtume (Salallah Aalayhi Wassalaam) alionekana akipaka udhu kichwa kizima na pamoja na shingo?

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu kupaka maji wakati wa kuchukua wudhuu kichwa kizima pamoja na shingo. Hakika ni kuwa hakuna Hadiyth iliyo sahihi kuonyesha kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alifanya hivyo wakati wa kuchukua wudhuu. Hivyo ndivyo alivyosema Ibn Taymiyah (Rahimahu Allaah) katika kitabu cha Majmuu’ al-Fatawaa na Ibn al-Qayyim al-Jawziyah (Rahimahu Allaah) katika kitabu chake Zaad al-Ma’ad. Imaam An-Nawawiy (Rahimahu Allaah) naye katika kitabu chake Al-Majmu’ ameeleza pia kuwa hakuna katika mapokezi ya Imaam Ash-Shaafi’iy kuwa alisema kupangusa shingo wakati wa wudhuu ila baadhi ya wafuasi wake ndio waliokuja na fikra hiyo. Pia anasema Imaam An-Nawawiy (Rahimahu Allaah) kuwa hilo si katika mafundisho ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na katika mafundisho ya wudhuu ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yaliyoelezewa na Khaliyfah ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Radhiya Allaahu ‘anhu) hakuna popote kuna kupangusa au kuosha shingo. Hivyo, si katika Sunnah kupangusa shingo wakati wa kuchukua wudhuu. Na Allaah Anajua zaidi






Vitambulisho:




Wanaostahiki kupewa Zaaka na kutowa Zaaka