Kuwagharimia Wazazi Kwenda Hajj Kabla Ya Kufanya Mwenyewe


382

SWALI LA KWANZA:

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho Tunashukuru kwa maswali hayo muhimu. Hija ni wajibu kwa kila Muislam aliyebaleghe na mwenye uwezo na akili timamu, hivyo basi, inahitajika kwanza wanaotaka kuwatumia gharama wazazi wao ili wafanye fardhi hii, wao kwanza waifanye ibada hiyo kabla ya kumpeleka au kumgharamia mwengine. Na kutoitekeleza fardhi hii bila ya udhuru itakuwa ni kumuasi Mola Mtukufu na pia ni dhambi. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala): ((وَلِلّهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلاً وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ الله غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ)) ((Na kwa ajili ya Allaah imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea. Na atakayekanusha basi Allaah si mhitaji kwa walimwengu)) [Al-'Imraan: 96-97] Ikiwa mtu ameweka nia kumpeleka mzazi wake Hajj kwa kumtumia gharama ili akaifanye mwenyewe, basi inaweza kukubalika ikiwa mtu huyo ana udhuru wa kutoweza kwenda mwaka huo. Ama kumfanyia Hajj mtu mwengine au kumgharamia na hali mwenyewe hakuifanya basi haifai hadi awe kwanza mwenyewe keshaifanya. Ifahamike kuwa kila mtu siku ya Qiyaamah atahukumiwa kwa 'amali zake na 'amali zake ndizo zitakazohesabiwa kwanza na si za wengine kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala): ((أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَى)) ((وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلَّا مَا سَعَى)) ((وَأَنَّ سَعْيَهُ سَوْفَ يُرَى)) (( ثُمَّ يُجْزَاهُ الْجَزَاء الْأَوْفَى)) ((Ya kwamba haichukui nafsi dhambi za nafsi nyingine)) ((Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyoyafanya mwenyewe)) ((Na kwamba vitendo vyake vitaonekana)) ((Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa ukamilifu)) [An-Najm:38-41] Wala hakuna yeyote atakayebeba dhambi au mema ya mwingine; si wazazi wala ndugu wala jamaa yeyote: ((وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَى وَإِن تَدْعُ مُثْقَلَةٌ إِلَى حِمْلِهَا لَا يُحْمَلْ مِنْهُ شَيْءٌ وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَى)) ((Wala hatabeba mbebaji mzigo wa mwingine. (Kila mtu atachukua jukumu ya dhambi zake mwenyewe). Na kama aliyetopewa na mzigo wake akimwita (mwingine) kwa ajili ya mzigo wake (amchukulie) hautachukuliwa hata kidogo (na mtu huyo) inagawa ni jamaa yake)) [Faatwir:18] Vilevile hatujui mtu uhai wake una muda gani, lini atachukuliwa na Mola wake. Hivyo inahitajika zaidi mtu aharakishe kwanza kujifanyia Hija mwenyewe kabla ya kumfanyia mtu mwengine hata ikiwa ni wazazi wake. Ile itikadi walionayo wengi wetu kuwa mama ni mkubwa kiumri na anaweza kuondoka kabla ya mwanawe, ni itikadi isiyo sahihi kwa sababu hakuna anayejua siku yake ya kufa na hakuna mwenye kujua ataishi umri gani, kwani mauti hayana mdogo wala mkubwa. Ushauri wetu ni kuwa, ikiwa hakuna kizuizi chochote cha mtu kufanya Hija mwaka huu, basi waharakishe wao kuitekeleza kwanza na waweke nia inshaAllaah mwakani kuwagharamia au kuwafanyia mzazi/wazazi. Baadhi ya Maulamaa wamesema kuwa udhuru wa kukosa Mahram unakubalika kwa Mwanamke kutokwenda Hajj. Hivyo ikiwa hii ni hali ya muulizaji, basi anaweza kumgharimia mzazi wake kwenda Hajj kisha atakapopata tu yeye mahram atie nia ya kwenda. Na mama naye aliyekuwa hana uwezo kama ilivyokuwa hali ya muulizaji wa pili, basi naye hana wajibu wa kutekeleza Hajj kwani fardhi hii ni kwa wale wenye uwezo tu kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala): ((وَلِلّهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلاً)) ((Na kwa ajili ya Allaah imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea)) [Al-'Imraan: 96-97] Wa Allaahu A'alam






Vitambulisho:




MIONGONI MWA DALILI   ZA UTUME WAKE (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam)