Maana Ya Janaba, Na Kuoga Janaba Kwa Asiyeoa


796

SWALI: Assalaamu alaikum, Je nani anaruhusiwa kukoga janaba kati ya mtu kisha oa na mwenye ajaoa (ao ajaolea)? Na nini maana ya janaaba kwa ufupi ao kujitwayarisha? Masalam Assalaamu alaikum,

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu janaba. Janaba ni hali ya mwanamme au mwanamke kutoa maji (manii) kutika uchi wake wa mbele au kujimai mume na mke, ikiwa watashusha (kutoa manii) au bila kushusha maadam zimekutana tupu zao mbili kwa kuingiliana. Kwa asiyeoa au kuolewa ipo njia moja tu ya kimaumbile ambayo anaweza kupata janaba nayo ni kuota na kisha kutoa maji ya manii ima akiwa amelala au akiwa macho. Na ama akiwa ameoa au ameolewa basi kule kujamiiana kunawafanya wote wawili wawe katika hali ya janaba. Ikiwa mume amecheza na mkewe bila kujimai naye, yeye pekee akashusha au wote wawili, basi katika hali hiyo, mume pekee au wote wawili watakuwa katika janaba. Mtu ambaye ana janaba inabidi ajitwahirishe ili aweze kutekeleza ‘Ibaadah zote anazohitajika kuzitekeleza. Na kuoga josho la janaba ni kujimwagia maji mwili mzima (kila sehemu ya mwili ipate maji). Njia hii ni kwa ufupi kama ulivyotaka. Ama kwa urefu ni kuwa unaosha vitanga vyako vya mkono, kisha unachukua wudhuu kama wudhuu wa Swalah pamoja na kuosha miguu yako au bila kuosha. Baada ya hapo utatia maji kichwani uhakikishe yamefika mpaka utosini mara tatu. Kisha utaanza kujimwagia maji upande wa kulia kisha wa kushoto. Sehemu zenye mikunjo inabidi upitishe maji yaenee hata zile sehemu za ndani. Kufanya hivyo utakuwa umeoga janaba na wakati huo utakuwa twahara. Ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi: Ghuslu - Vipi Kukoga Janabah, Nifaas Na Hedhi Na Allaah Anajua zaidi






Vitambulisho:




Kutayamamu