JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani kwa swali lako kuhusu utoaji wa Zakaah. Hakika Zakaah inatolewa kwa akiba iliyoiweka ikafikiwa na kiwango cha chini cha kutolewa Zakaah; kiwango hicho huitwa ‘Niswaab’, pia dhahabu na fedha na wanyama wa mifugo na mazao ya ukulima. Katika tulivyovitaja juu vina masharti mawili makuu ili kupaswa kutolewa zakaah. Masharti yenyewe ni: 1. Kufikiwa na Niswaab (kiwango cha chini cha kutolewa Zakaah). Kwa pesa taslimu ni kuwa na akiba inayoweza kununua gramu 85 ya dhahabu safi. Na dhahabu ni kuwa na gramu 85 ilhali fedha ni gramu 595. Ama wanyama inategea kwa mbuzi na kondoo ni kuwa na idadi iliyo 40 ilhali ngamia ni 5. Na mazao ni wakati wa kuvuna. 2. Kupitiwa na Hawl (mwaka mzima katika kalenda ya Kiislamu). Ama ikiwa una nyumba au gari au vyombo vya nyumbani hivi havitolewi Zakaah ila ikiwa ni vya biashara. Ikiwa nyumba umeikodisha au gari linafanyiwa kazi utaanza kulipa tu Zakaah ikiwa katika akiba kwa unachopata itafikia kiwango cha kutolewa Zakaah basi itabidi ufanye hesabu kwa unachopata katika mapato yako. Na wakati inafika Niswaab utaweka hiyo tarehe kwani ikifika mwaka unaofuatia ikiwa bado iko katika kiwango hicho au zaidi itabidi utoe 2½% ya akiba hiyo kuwapatia wale waliotajwa katika Suratut Tawbah 9: aayah 60. 2. Kupitiwa na Hawl (mwaka mzima katika kalenda ya Kiislamu). Ama ikiwa una nyumba au gari au vyombo vya nyumbani hivi havitolewi Zakaah ila ikiwa ni vya biashara. Ikiwa nyumba umeikodisha au gari linafanyiwa kazi utaanza kulipa tu Zakaah ikiwa katika akiba kwa unachopata itafikia kiwango cha kutolewa Zakaah basi itabidi ufanye hesabu kwa unachopata katika mapato yako. Na wakati inafika Niswaab utaweka hiyo tarehe kwani ikifika mwaka unaofuatia ikiwa bado iko katika kiwango hicho au zaidi itabidi utoe 2½% ya akiba hiyo kuwapatia wale waliotajwa katika Suratut Tawbah 9: aayah 60.