Muajiriwa Kazi Anayepokea Kila Mwezi Anatakiwa Atoe Zakaah?


481

SWALI: Assalam alaikum w.w? Swali langu ni kuhusu Zakaah. Je kama sisi wenye mshahara kwa mwezi mfano anae pokea alfu hamsini 50.000 Za Rwanda (Dollar 100 ni 55.000Frw), ao mwenzangu anae pokea 120.000 Frw ivo Zakaah yetu itatolewa kivipi kwa hesabu? Hatuna nyumba wala cocote ni mshahara peke yake.Tunaomba kama inawezekana tupewe vile tutakavyo lipa hio Zakaah tusije kesho kufanya makosa na alhidaaya imeisha kuwa karibu na si

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kutoa Zakaah kwa muajiriwa anayelipwa kila mwezi Kwanza kabisa tunapenda kuwakumbusha wote wenye kuzoea kufupisha Salaam au kufupisha kumswalia Mtume wetu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) au kufupisha kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), ni bora waache kufanya hivyo na waandike kwa urefu kwani zote hizo ni 'Ibaadah na ni bora kuzifanya kwa ukamilifu ikiwemo katika kuandika, kutamka n.k. Pia kuongeza neno 'Ta'ala' kwenye Salaam kwa kusema 'Assalaamu 'Alaykum wa RahmatuLlaahi Ta'ala wa Barakaatuh', si jambo tulilofundishwa katika Salaam na hivyo ni bora mtu kuliepuka katika Salaam. Kila jambo katika Uislamu lina masharti yake na Zakaah si tofauti na ‘amali nyingine. Ama masharti ya kumpasa mtu kutoa Zakaah ni: 1. Kufika nisaab (kiwango cha chini ya kulazimika kutoa Zakaah). Kiwango hicho ni mtu kuwa na akiba ya fedha taslimu zenye thamani sawa na gramu 82.5 ya dhahabu. 2. Akiba hiyo iliyofika nisaab kupitiwa na mwaka katika kalenda ya Kiislamu. Tukichukulia hiyo mishahara uliyotoa kama mfano hiyo si akiba yako bali unafaa kutoa ajira ya nyumba, chakula, bili za nyumba, umeme, maji na matumizi na kadhalika. Hata hivyo, kutakuwa na akiba ambayo unabakisha kila mwezi. Hii akiba unayoweka itakuwa inaongezeka kila mwezi mpaka kufikia nisaab ikiwa hakutatokea lolote la kukufanya uzitumie. Ile tarehe ambayo akiba yako itafikia nisaab ndio utaanza kuhesabu mwaka kuanzia tarehe hiyo. Na itakapotimia mwaka tokea uanze kukusanya pesa zako, basi utatoa 2½% ya pesa zako kama Zakaah yako. Na Allaah Anajua zaidi






Vitambulisho: