Mwanamke Mwenye Hedhi Anaweza Kuingia Katika Chumba Cha Kuswalia?


333

SWALI: Assalam aleykum warahamatullahi wabarakatu swali langu la leo ni kuwa hapa chuo naposoma waislamu tumejiunga na tumeanzisha chama cha kufundishana kuhusu Uislam, hapa hostel tunasehemu inaitwa prayer room.. sasa swali langu linauliza je mimi kama mwanamke naruhusiwa kuingia kwenye prayer room wakati nikiwa katika hedhi, pale napokutana na Waislamu wenzangu??

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuingia katika Prayer room wakati wa hedhi. Ikiwa ni dharura kama hiyo ya kukutana na wenzako kwa sababu moja au nyingine huruhusiwa kuingia hata katika Msikiti licha ya hicho chumba mlichopatiwa kwa ajili ya Swalah. Hivyo, kukiwa na dharura kama kwenda kupata elimu, kusikiliza darsa, kuchukua kitu, kumtafuta mtu n.k. basi unaweza kuingia na baada ya dharura kumalizika utatoka. Anachotakiwa ni kuvaa vizuizi vizuri sehemu zake siri ili asije kuchafua sehemu hiyo. Na Allaah Anajua zaidi






Vitambulisho: