Ni Lazima Kutumia Shampoo Na Sabuni Katika Kujitia Twahara (Ghusl?)


435

SWALI: Aaw - swali langu ni hili unapooga janaba ni lazima nywele uzioshe na shampoo au unapotia maji mwili mzima na kichwa inatosha kwani nywele wakati mwingine si chafu unakuwa umeosha karibuni. Asalam alekum. SWALI LA PILI: Assalamu_alayku. Mimi suala langu niuliza yakwamba: Nib ipi hukmu ya mwenye kukoga kwa ajili ya kujitoharisha(janaba, hedhi ) na huku wakati anapokoga anajipaka sabuni?

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Hakika tunakushukru dada yetu kwa swali lako kuhusu mas-ala ya kuoga josho la janaba. Tunakukumbusha pia wewe na ndugu zetu wengine wawe ni wenye kuandika Salaam kwa ukamilifu kama tulivyofundishwa na Mtume wetu kipenzi (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na akatujulisha thawabu zake. Hivyo kufupisha namna hiyo “Aaw” au “A.A.W.W” ni mambo ambayo hatujafundishwa na pia yanatukosesha thawabu zilizotajwa. Tukijibu swali lako, Uislamu kusahilisha mambo umeweka kanuni ambazo zitaweza kutekelezwa na wafuasi wake wakiwa katika pembe zote za ulimwengu. Ndio Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Akatuambia: Wala Hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini” (22: 78). Hivyo katika mas-ala ya kuoga janaba kunapatika nguzo mbili muhimu, nazo ni: Kutia nia, na Kujimwagia na kujisafisha maji mwili mzima. Mambo hayo yakishafanyika kunakuwa hakuna haja ya kutia shampoo au sabuni lakini ukitaka kujipaka sabuni au shampoo hakuna tatizo lolote, bali ni vizuri zaidi kwani kujisafisha na sabuni na kuosha nywele kwa shampoo huleta usafi zaidi na khaswa wakati mtu ametoka katika hedhi. Na Allaah Anajua zaidi






Vitambulisho:




Injili ya Mathayo