JIBU: Sifa zote njema anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shari'ah inakuruhusu kula ikiwa unakhofu kuwa Swawm itakufanya ukose maziwa ya kumnyonyesha mtoto. Kisha unatakiwa ulipe deni lako baada ya Ramadhaan. Na ikiwa utashindwa kulipa hadi Ramadhaan nyingine, Wanachuoni wametofautiana kuhusu kulipa kafara; wako wanaoonelea kuwa utalipa Swawm na kutoa kafara, na wako wanaoonelea kuwa utalipa tu Swawm zako bila kutoa kafara. Na hii rai ya pili ina nguvu zaidi. Kwa maelezo zaidi tafadhali ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi kuhusu maudhui hiyo: Kulipa Swawm Na Kafara Na Allaah Anajua zaidi