Sajda Ya Kusahau Inapasa Katika Swalaah Za Sunnah?


351

SWALI: Assalam alaykum Namshukuru Allah kwa kila kitu, na pia natarajia kuwa mnaendelea kwa afya njema na uzima kamili pamoja na shughuli zote za dawa. Nimefurahi kujibiwa lile suali langu la chakula cha halali. Pia leo nna masuali haya - Katika Swala, tunaposali, Mtume wetu na kipenzi chetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametufundisha Sijidatusahau pindi tunaposahau katika raka au na mengi. Jee hizi sijidatu sahau zinatumika kwenye sala za Sunna pia. Ahsanteni sana na Allah Akuwafikishieni kheri Duniani na Akhera. Amin.

JIBU: AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho. Sajdatus-sahw (sujudu ya kusahau) inafanywa kukamilisha kilichosahauliwa sawa ikiwa ni katika Swalaah ya faradhi au ya Sunnah kwani dalili zimekuja kwa njia ya ujumla. Mfano ni kauli ya Rasuli wa Allah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pale aliposema: “Anaposahau mmoja wenu, asujudu sijda mbili" [Muslim kutoka kwa Ibn Mas-‘uwd [Radhwiya Allaahu 'anhu]). Na Allaah Anajua zaidi






Vitambulisho:




Abdullah Al Matrood - Quran Downloads