Swalaah Za Sunnah Lazima Zisomwe Na Surah?


570

SWALI: Suna waweza sali bila kusoma sura 2? Maana huku nilipo ughaibuni naona wenzetu wa Senegal na Gambia mtu anakim swala tu kesha kwenda kusugud nashindwa kuelewa hili.

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kusoma surah ya pili katika Swalah za Sunnah. Hakika ni kuwa si lazima kusoma surah ya pili baada ya Suratul Faatihah. Hata hivyo, katika Swalah za Sunnah nyingine maelekezo na matendo ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yaonyesha kuwa alikuwa haachi kusoma Surah ya pili. Mfano wa hilo, ni katika Sunnah ya rakaa mbili kabla ya Alfajiri na Swalah ya Witr. Na kwa kuwa yeye mwenyewe (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuambia: “Swalini kama mlivyo niona nikiswali” (Al-Bukhaariy). Yatakiwa nasi katika Swalah hizo tufuate mwendo huo. Jambo ambalo hatukulielewa ni kipengele cha pili cha swali lako: “Maana huku nilipo ughaibuni naona wenzetu wa Senegal na Gambia mtu anakim swala tu kesha kwenda kusugud nashindwa kuelewa hili”. Kuswali kwa haraka namna hiyo hatuelewi ni kitu gani lakini msingi na wajibu mkubwa wa Swalah ni utulivu katika kila kituo. Ikiwa haraka ni namna hiyo ya kukimu na mara moja mtu yuko katika sajdah, hilo litakuwa ni kosa na hiyo si Swalah. Na Allaah Anajua zaidi






Vitambulisho:




Qur-aan ….Kitabu cha Mwisho cha Mbinguni.