Swawm Ya Arafah Ipi Sahihi Kufunga Kwa Kuwafuata Hujaji Au Kufuata Nchi Uliyoko


296

SWALI: ASSALAAM ALAYKUM NDUGU ZANGU KATIKA IMANI NAOMBA KUULIZA KATI YA MWEZI TISA NA MWEZI NANE NI SIKU GANI NI SAHIHI KUFUNGA ARAFA? NAOMBA UFAFANUZI WENU

JIBU: AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho. Swawm ya ‘Arafah, usahihi wake ni siku wanayosimama Hujaaj katika viwanja vya ‘Arafah huko Makkah. Na siku hiyo ni siku ya tisa ya Hajj. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swawm ya 'Arafah nataraji (kwa Allaah) kufuta madhambi ya mwaka uliopita na wa baada yake.” [Muslim] Katika Hadiyth hiyo, ni wazi kabisa na dalili isiyo shaka kuwa Swawm ya ‘Arafah inakuwa ni katika siku ya ‘Arafah. Na ‘Arafah ni jina la sehemu, na sehemu yenyewe iko Makkah pale ambapo Hujaaj wanasimama kisimamo cha siku ya tisa ya Hijjah. Kwa hiyo, mtu atapofunga siku ambayo Hujaaj hawapo ‘Arafah, basi hiyo haitoitwa Swawm ya ‘Arafah. Pamoja na kwamba kuna baadhi ya Wanachuoni wanaoonelea kuwa watu wafuate tarehe tisa za nchi zao au za mwandamo wao, lakini hiyo ni rai ambayo si sahihi. Na rai sahihi ni hiyo inayowafikiana na hiyo Hadiyth iliyo wazi kabisa hapo juu. Kwa hiyo, Swawm hiyo ya ‘Arafah huwa tarehe tisa ya mwezi wa Dhul-Hijjah, siku ambayo Hujaaj wanasimama katika viwanja vya ‘Arafah huko Makkah. Na Allaah ni Mjuzi zaidi






Vitambulisho:




Fares Abbad - Quran Downloads