Tofauti Baina Ya Manii Na Madhii Na Hukumu Zake Za Ghuslu


457

SWALI mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 25 na sijaolewa na pia ni mwislam safi na najiamini na pia nina imani katika dini yangu na namwomba MWENYEZI MUNGU anizidishie mimi na wewe INSHAALAAH NA WAISLAM WOTE AMINI. ninatatizo moja nalo ewe utakayesoma naomba nistiri. huwa nakuwa nikitokwa na manii mara kwa mara hata kama sijawaza au kutamani map

JIBU: BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu wa Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa ba’ad: Inaonyesha kutokana na usemi wako kwamba yanayokutoka ni 'madhiy' na sio 'maniy'. Na kuna tofauti katika vitu hivi viwili kama ifuatavyo: A-Tofauti zao kuhusu sifa zake: Manii Shahawa (manii) ya mwanamume ni maji meupe mazito. Kwa mwanamke ni ya rangi ya manjano na mepesi. Manii kwa kawaida huwa ni maji yanayotokwa kwa mwanamume au mwanamke wakati wa kilele cha raha wakati wa mapenzi. Dalili ya sifa hiyo ya manii ni kutoka: عن أم سليم رضي الله عنها أنها سألت نبي الله صلى الله عليه وسلم عن المرأة ترى في منامها ما يرى الرجل . فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم : " إذا رأت ذلك المرأة فلتغتسل " فقالت أم سليم : - واستحيَيْتُ من ذلك - قالت : وهل يكون هذا ؟ . فقال النبي صلى الله عليه وسلم : " فمن أين يكون الشبه ؟ إن ماء الرجل غليظ أبيض وماء المرأة رقيق أصفر فمن أيهما علا أو سبق يكون الشبه " متفق عليه Hadiyth ya Ummu Sulaym رضي الله عنها ambaye alimuuliza Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kama mwanamke mwenye kuota ndoto ya kujimai inampasa afanye ghuslu. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alisema "Ndio ikiwa ataona maji".Ummu Sulaym akasema: "Niliona haya niliposikia hivyo nikauliza: "Inawezekana hivyo?" Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema: "Vipi basi mtoto atamshabihi baba yake au mama yake? Maji ya mwanamume ni mazito na meupe na maji ya mwanamke ni mepesi na manjano. Yoyote kati ya hayo yatakayotoka mwanzo ndio yanayosababisha mzazi gani awe ni mwenye kumshabihi mtoto" [Al-Bukhaariy Na Muslim] Sifa zifuatazo tatu ndizo zenye kujulisha manii ya mwanamume: 1. Kutoka kwake kunaambatana na kilele cha raha na kufuatilia uchovu. 2. Harufu yake ni kama chavuo (pollen) ya mtende ambayo huwa kama harufu ya unga uliokandwa. 3. Hutoka kwa kububujika kwa nguvu. Mojawapo katika sifa hizo inatosha kutambulisha kuwa ni manii. Ikiwa mtu ametokwa na maji na hazikupatikana sifa hizo basi hayatakuwa ni manii. Sifa mbili za manii ya mwanamke: 1. Yana harufu kama harufu ya manii ya mwanamume. 2. Kutokwa kwake kunaambatana na hisia ya kilele cha raha na hufuatilia na uchovu. Madhiy Madhiy ni maji yenye kunata na yanamtoka mtu aidha anapokuwa anawaza au kutamani kujimai, au hata bila ya kuwaza kama ilivyo katika hali ya muulizaji. Na hazina sifa kama sifa za manii tulizozitaja hapo juu. Na pia huwatokea wanawake na wanaume ila aghlabu huwatokea sana wanawake. (Hii ni rai ya Imaam An-Nawawiy katika maelezo yake ya Sharh Muslim 3/213 B-Tofauti kuhusu ya hukumu yake baada ya kutokwa Manii: Yanapotoka manii, inampasa mtu afanye ghuslu kwa ajili ya kujitoharisha (janaabah) ikiwa yamemtoka mtu manii wakati wa kujimai au kwa hali yoyote nyingine ikiwa yu macho au ameota ndoto n.k. Madhiy Yanapomtoka mtu madhiy humpasa kufanya wudhuu tu. Na dalili ni: ((ما رواه علي بن أبي طالب رضي الله عنه قال : كنت رجلا مذّاء فأمرت المقداد أن يسأل رسول الله صلى الله عليه وسلم فسأله فقال : " فيه الوضوء ")) متفق عليه ((Kutoka kwa 'Aliy bin Abi Twaalib رضي الله عنه ambaye amesema: "Nilikuwa ni mtu niliyekuwa nikitokwa sana na maji ya urethra (madhii). Nikamuambia Miqdaad amuulize Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kuhusu hilo. Akamuuliza na akasema: "Inahiitajika kufanya wudhuu")) [Al-Bukhaariy na Muslim] C-Tofauti kama ni najisi au ni tohara Manii Manii ni tohara kutokana na rai za Maulamaa ambao wamechukua dalili kutokana na mapokezi yafuatayo: ((عن عائشة رضي الله عنها قالت : "كان رسول الله صلى الله عليه وسلم يغسل المني ثم يخرج إلى الصلاة في ذلك الثوب وأنا أنظر إلى أثر الغسل فيه")) . متفق عليه ((Kutoka kwa Bibi 'Aishah رضي الله عنها ambaye amesema: "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikuwa akikosha manii (yaliyokuwa katika nguo yake) kisha akienda kuswali akiwa ameivaa nguo hiyo na nilikuwa naona sehemu aliyoiosha")) [Al-Bukhaariy na Muslim] وفي رواية لمسلم " ولقد كنت أفركه من ثوب رسول الله صلى الله عليه وسلم فركا فيصلي فيه Kutokana na mapokezi yaliyosimuliwa na Muslim "Nilikuwa nikiyafikicha vizuri (manii) kutoka nguo ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kisha akiiswalia" (hiyo nguo). وفي لفظ " لقد كنت أحكّه يابسا بظفري من ثوبه " Na usemi mwingine: "Nilikuwa nikiikwaruza kutoka katika nguo kwa makucha yangu baada ya kukauka". بل ثبت أن النبي صلى الله عليه وسلم كان يترك غسله وهو رطب ويكتفي بمسحه بعود ونحوه كما روى الإمام أحمد في مسنده عن عائشة رضي الله عنه قالت : "كان رسول الله صلى الله عليه وسلم يسلت " يزيل ويميط " المني من ثوبه بعرق الأذخر ثم يصلي فيه ويَحتّه من ثوبه يابسا ثم يصلي فيه " ورواه ابن خزيمة في صحيحه وحسنه الشيخ الألباني في الإرواء. Imethibitika kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikuwa akiyaacha bila ya kuyaosha na yalikuwa bado maji maji, ilitosheleza kuyafuta kwa kijiti kama ilivyosimuliwana Imaam Ahmad katika Musnad yake kutoka kwa 'Aishah رضي الله عنها ambaye amesema: "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikuwa akiyaondosha manii katika nguo yake kwa mche wa adhkhar (aina ya mti), kisha akiiswalia nguo, kisha akiyafikicha baada ya kukauka na akiiswalia nguo hiyo hiyo" [Ibn Khuzaymah na Shaiyk Al-Albaaniy ameipa daraja ya Hasan katika Al-Irwaa ] Madhii Madhii ni najisi kutokana na Hadiyth: أن النبي صلى الله عليه وسلم أمر بغسل الذكر والأنثيين ( أي الخصيتين ) ويتوضأ كما)) أخرجه أبو عوانة في مستخرجه وقال ابن حجر في التلخيص : وهذا إسناد لا مطعن فيه Kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم aliamrisha kuosha sehemu ya siri ya mwanamume kisha atawadhe)) [Imesimuliwa na Abu 'Awaanah katika Al-Mustakhraj – Ibn Hajar kasema katika Al-Talkhiys "Hakuna makosa katika isnaad hii'] Kwa hiyo madhii ni najisi na sehemu za siri zioshwe kwani yanatengua tohara. D- Kuhusu nguo zilizoingia manii na madhii Manii Kwa vile manii ni tohara, basi yatakapoingia katika nguo hayafanyi nguo kuwa ni najisi, na anaweza mtu kuswalia nayo nguo hiyo. Lakini ni bora kuyafuta kama alivyosema Ibn Qudaamah katika Al-Mughni "Hata kama inasemekana kuwa manii ni tohara, lakini ni bora kuyafuta, lakini mtu akiswalia nayo Swalah itaswihi. Madhii Madhii yakiingia katika nguo inatosheleza kurashia maji juu yake kwa sababu kuepusha mashaka ya kuoga kila mara, kwani dini yetu ni nyepesi. Na dalili ni kutoka katika Hadiyth عن سهل بن حنيف قال : كنت ألقى من المذي شدة وكنت اكثر من الاغتسال فسالت رسول الله صلى الله عليه وسلم عن ذلك فقال " إنما يجزئك من ذلك الوضوء . قلت : يا رسول الله فكيف بما يصيب ثوبي منه ؟ قال : يكفيك بأن تأخذ كفاً من ماء فتنضح بها ثوبك حيث تُرى أي تظنّ أنه أصابه " ورواه الترمذي وقال الألباني : هذا حديث حسن Kutoka kwa Sahl ibn Haniyf ambaye amesema: "Nilikuwa nikitokwa na madhii na nilikuwa nikifanya ghuslu kila mara. Nikamuuliza Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema: "Inakutosheleza kufanya wudhuu" Nikasema: "ewe Mjumbe wa Allaah, vipi yakiingia katika nguo yangu?" Akasema: "Inakutosheleza kuchukua maji mkononi na kurashia juu ya nguo zako popote unapodhani (kuna madhiy")) [At-Tirmidhiy na kasema Shaykh Al-Albaaniy : Hadiyth,Hasan] Ili kutatua mushkila wako kuwa unatokwa na madhiy kila mara, ni bora kuvaa hifadhi nyepesi (panty-liners) au hata tissues ili ubakie safi katika nguo yako ya ndani na kila unapokwenda msalani kwa haja uwe unabadilisha. Kufanya hivi kutakuepusha na kurashia maji nguo yako ya ndani (underwear), na pia utakuwa unapata wepesi wa kutekeleza wudhuu wako. Na Allah Anajua zaidiJIBU: BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu wa Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa ba’ad: Inaonyesha kutokana na usemi wako kwamba yanayokutoka ni 'madhiy' na sio 'maniy'. Na kuna tofauti katika vitu hivi viwili kama ifuatavyo: A-Tofauti zao kuhusu sifa zake: Manii Shahawa (manii) ya mwanamume ni maji meupe mazito. Kwa mwanamke ni ya rangi ya manjano na mepesi. Manii kwa kawaida huwa ni maji yanayotokwa kwa mwanamume au mwanamke wakati wa kilele cha raha wakati wa mapenzi. Dalili ya sifa hiyo ya manii ni kutoka: عن أم سليم رضي الله عنها أنها سألت نبي الله صلى الله عليه وسلم عن المرأة ترى في منامها ما يرى الرجل . فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم : " إذا رأت ذلك المرأة فلتغتسل " فقالت أم سليم : - واستحيَيْتُ من ذلك - قالت : وهل يكون هذا ؟ . فقال النبي صلى الله عليه وسلم : " فمن أين يكون الشبه ؟ إن ماء الرجل غليظ أبيض وماء المرأة رقيق أصفر فمن أيهما علا أو سبق يكون الشبه " متفق عليه Hadiyth ya Ummu Sulaym رضي الله عنها ambaye alimuuliza Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kama mwanamke mwenye kuota ndoto ya kujimai inampasa afanye ghuslu. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alisema "Ndio ikiwa ataona maji".Ummu Sulaym akasema: "Niliona haya niliposikia hivyo nikauliza: "Inawezekana hivyo?" Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema: "Vipi basi mtoto atamshabihi baba yake au mama yake? Maji ya mwanamume ni mazito na meupe na maji ya mwanamke ni mepesi na manjano. Yoyote kati ya hayo yatakayotoka mwanzo ndio yanayosababisha mzazi gani awe ni mwenye kumshabihi mtoto" [Al-Bukhaariy Na Muslim] Sifa zifuatazo tatu ndizo zenye kujulisha manii ya mwanamume: 1. Kutoka kwake kunaambatana na kilele cha raha na kufuatilia uchovu. 2. Harufu yake ni kama chavuo (pollen) ya mtende ambayo huwa kama harufu ya unga uliokandwa. 3. Hutoka kwa kububujika kwa nguvu. Mojawapo katika sifa hizo inatosha kutambulisha kuwa ni manii. Ikiwa mtu ametokwa na maji na hazikupatikana sifa hizo basi hayatakuwa ni manii. Sifa mbili za manii ya mwanamke: 1. Yana harufu kama harufu ya manii ya mwanamume. 2. Kutokwa kwake kunaambatana na hisia ya kilele cha raha na hufuatilia na uchovu. Madhiy Madhiy ni maji yenye kunata na yanamtoka mtu aidha anapokuwa anawaza au kutamani kujimai, au hata bila ya kuwaza kama ilivyo katika hali ya muulizaji. Na hazina sifa kama sifa za manii tulizozitaja hapo juu. Na pia huwatokea wanawake na wanaume ila aghlabu huwatokea sana wanawake. (Hii ni rai ya Imaam An-Nawawiy katika maelezo yake ya Sharh Muslim 3/213 B-Tofauti kuhusu ya hukumu yake baada ya kutokwa Manii: Yanapotoka manii, inampasa mtu afanye ghuslu kwa ajili ya kujitoharisha (janaabah) ikiwa yamemtoka mtu manii wakati wa kujimai au kwa hali yoyote nyingine ikiwa yu macho au ameota ndoto n.k. Madhiy Yanapomtoka mtu madhiy humpasa kufanya wudhuu tu. Na dalili ni: ((ما رواه علي بن أبي طالب رضي الله عنه قال : كنت رجلا مذّاء فأمرت المقداد أن يسأل رسول الله صلى الله عليه وسلم فسأله فقال : " فيه الوضوء ")) متفق عليه ((Kutoka kwa 'Aliy bin Abi Twaalib رضي الله عنه ambaye amesema: "Nilikuwa ni mtu niliyekuwa nikitokwa sana na maji ya urethra (madhii). Nikamuambia Miqdaad amuulize Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kuhusu hilo. Akamuuliza na akasema: "Inahiitajika kufanya wudhuu")) [Al-Bukhaariy na Muslim] C-Tofauti kama ni najisi au ni tohara Manii Manii ni tohara kutokana na rai za Maulamaa ambao wamechukua dalili kutokana na mapokezi yafuatayo: ((عن عائشة رضي الله عنها قالت : "كان رسول الله صلى الله عليه وسلم يغسل المني ثم يخرج إلى الصلاة في ذلك الثوب وأنا أنظر إلى أثر الغسل فيه")) . متفق عليه ((Kutoka kwa Bibi 'Aishah رضي الله عنها ambaye amesema: "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikuwa akikosha manii (yaliyokuwa katika nguo yake) kisha akienda kuswali akiwa ameivaa nguo hiyo na nilikuwa naona sehemu aliyoiosha")) [Al-Bukhaariy na Muslim] وفي رواية لمسلم " ولقد كنت أفركه من ثوب رسول الله صلى الله عليه وسلم فركا فيصلي فيه Kutokana na mapokezi yaliyosimuliwa na Muslim "Nilikuwa nikiyafikicha vizuri (manii) kutoka nguo ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kisha akiiswalia" (hiyo nguo). وفي لفظ " لقد كنت أحكّه يابسا بظفري من ثوبه " Na usemi mwingine: "Nilikuwa nikiikwaruza kutoka katika nguo kwa makucha yangu baada ya kukauka". بل ثبت أن النبي صلى الله عليه وسلم كان يترك غسله وهو رطب ويكتفي بمسحه بعود ونحوه كما روى الإمام أحمد في مسنده عن عائشة رضي الله عنه قالت : "كان رسول الله صلى الله عليه وسلم يسلت " يزيل ويميط " المني من ثوبه بعرق الأذخر ثم يصلي فيه ويَحتّه من ثوبه يابسا ثم يصلي فيه " ورواه ابن خزيمة في صحيحه وحسنه الشيخ الألباني في الإرواء. Imethibitika kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikuwa akiyaacha bila ya kuyaosha na yalikuwa bado maji maji, ilitosheleza kuyafuta kwa kijiti kama ilivyosimuliwana Imaam Ahmad katika Musnad yake kutoka kwa 'Aishah رضي الله عنها ambaye amesema: "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikuwa akiyaondosha manii katika nguo yake kwa mche wa adhkhar (aina ya mti), kisha akiiswalia nguo, kisha akiyafikicha baada ya kukauka na akiiswalia nguo hiyo hiyo" [Ibn Khuzaymah na Shaiyk Al-Albaaniy ameipa daraja ya Hasan katika Al-Irwaa ] Madhii Madhii ni najisi kutokana na Hadiyth: أن النبي صلى الله عليه وسلم أمر بغسل الذكر والأنثيين ( أي الخصيتين ) ويتوضأ كما)) أخرجه أبو عوانة في مستخرجه وقال ابن حجر في التلخيص : وهذا إسناد لا مطعن فيه Kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم aliamrisha kuosha sehemu ya siri ya mwanamume kisha atawadhe)) [Imesimuliwa na Abu 'Awaanah katika Al-Mustakhraj – Ibn Hajar kasema katika Al-Talkhiys "Hakuna makosa katika isnaad hii'] Kwa hiyo madhii ni najisi na sehemu za siri zioshwe kwani yanatengua tohara. D- Kuhusu nguo zilizoingia manii na madhii Manii Kwa vile manii ni tohara, basi yatakapoingia katika nguo hayafanyi nguo kuwa ni najisi, na anaweza mtu kuswalia nayo nguo hiyo. Lakini ni bora kuyafuta kama alivyosema Ibn Qudaamah katika Al-Mughni "Hata kama inasemekana kuwa manii ni tohara, lakini ni bora kuyafuta, lakini mtu akiswalia nayo Swalah itaswihi. Madhii Madhii yakiingia katika nguo inatosheleza kurashia maji juu yake kwa sababu kuepusha mashaka ya kuoga kila mara, kwani dini yetu ni nyepesi. Na dalili ni kutoka katika Hadiyth عن سهل بن حنيف قال : كنت ألقى من المذي شدة وكنت اكثر من الاغتسال فسالت رسول الله صلى الله عليه وسلم عن ذلك فقال " إنما يجزئك من ذلك الوضوء . قلت : يا رسول الله فكيف بما يصيب ثوبي منه ؟ قال : يكفيك بأن تأخذ كفاً من ماء فتنضح بها ثوبك حيث تُرى أي تظنّ أنه أصابه " ورواه الترمذي وقال الألباني : هذا حديث حسن Kutoka kwa Sahl ibn Haniyf ambaye amesema: "Nilikuwa nikitokwa na madhii na nilikuwa nikifanya ghuslu kila mara. Nikamuuliza Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema: "Inakutosheleza kufanya wudhuu" Nikasema: "ewe Mjumbe wa Allaah, vipi yakiingia katika nguo yangu?" Akasema: "Inakutosheleza kuchukua maji mkononi na kurashia juu ya nguo zako popote unapodhani (kuna madhiy")) [At-Tirmidhiy na kasema Shaykh Al-Albaaniy : Hadiyth,Hasan] Ili kutatua mushkila wako kuwa unatokwa na madhiy kila mara, ni bora kuvaa hifadhi nyepesi (panty-liners) au hata tissues ili ubakie safi katika nguo yako ya ndani na kila unapokwenda msalani kwa haja uwe unabadilisha. Kufanya hivi kutakuepusha na kurashia maji nguo yako ya ndani (underwear), na pia utakuwa unapata wepesi wa kutekeleza wudhuu wako. Na Allah Anajua zaidi






Vitambulisho:




Ali Hajjaj Souissi