Ukisahau Kuosha Kiungo Kimoja Katika Wudhuu Ufanyeje?


292

SWALI: Ukisahau kuosha viganja vya mikono na umeosha uso mara moja, je unaweza kurudi kwenye mikono bila ya kuanza udhu upya?

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Ukisahau ukatia wudhuu kiungo kingine kabla ya kile kinachotakiwa ni bora kuanza wudhuu upya kwani ni katika sharti za wudhuu kufanya kwa mpangilio wake kuanza viganja vya mikono, kusukutua na pua, uso, mikono, kichwa na masikio na miguu. Na Allaah Anajua zaidi






Vitambulisho:




Ibrahim al-Dosari