Wakati Wa Mwisho Kukoga Janaba Katika Mwezi Wa Ramadhaan


334

SWALI: Asaalam alaykum, Ningependa kujua ni wakati gani wa mwisho naweza kukoga janaba katika mwezi wa Ramadhani

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), Mola wa viumbe vyote. Swala na salamu kwa kipenzi chetu, Nabii Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ahli zake na Masahaba zake na watu wema mpaka Siku ya Qiyaamah. Kuoga janaba katika mwezi wa Ramadhaan unaweza kufanya wakati wowote wa usiku au Alfajiri kabla ya jua la asubuhi kuchomoza ili uweze kuwahi kuswali Swalah ya Alfajiri. Ikiwa pia umelala mchana na ukaota na kupatikana na janaba ukiamka itabidi uoge ili uweze kuswali. Lakini ikiwa umepata janaba ukiwa macho ima kwa sababu ya matamanio au kupiga punyeto (tendo ni makosa hata ikiwa hukufunga) na ukatokwa na manii saumu yako inakuwa ni batili na hufai kula. Wa Allaahu A'alam






Vitambulisho:




Wanadamu ni Wanyama wanapokataa Dini.