Watoto Wakipita Mbele Ya Mwenye Kuswali Au Kumkalia Swalaah Inafaa?


283

SWALI: salam alaikum ndugu zangu waislam shukrani nyingi kwa alhidaaya inshaallahallah atakulipeni. suala langu ukitaka kuswali kama kuna watoto wadogo wanakupitia katika swalah mara wanakuja kukukalia je swalah yako iko sawa?

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukurani kwa swali lako kuhusu watoto wanaokuja mbele yako unaposwali. Unapaswa ujitahidi kadiri uwezavyo kuwazuia watoto wasipite mbele yako unaposwali au kucheza mbele yako. Unapaswa uswali karibu na ukuta au 'sutrah' kizuizi unachotakiwa uweke mbele yako ili mtu asipite mbele yako. Na ikiwa ni watoto wadogo wasiotambua kitu ambao umejaribu kuwazuia na hawasikii basi tafuta mtu wa kukaa nao hadi umalize Swalah. Ikiwa imeshindikana, basi Swalaah yako iko sawa kabisa kwani hali kama hiyo ilimtokea Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na wajuu wake Al-Hasan na Al-Husayn walipomjia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakimpandia juu ya mabega na mgongoni akiwaacha na kuendelea na Swalah yake. Hata hivyo, unapaswa ujitahidi kuwa makini kwani hali kama hizo huwa zinaondosha khushu'u ya mtu kwenye Swalaah yake na kumshughulisha. Na Allaah Anajua zaidi






Vitambulisho:




Hedhi, inayofanana na hedhi na nifasi