Wudhuu Unafaa Ukivaa Pete?


353

SWALI: Assalam alaikum, Swali langu ni hili: je mtu akitawadha na anavaa pete inayomubana nakisha aka suali suala inakubaliwa?

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Wudhuu ni msingi muhimu sana wa kukubaliwa kwa Swalah ya mtu, kwani Swalah haikubaliwi bila wudhuu. Katika kutawadha maji yanatakiwa yafike katika kila sehemu ya kiungo hicho. Ikiwa maji hayaingii sehemu Fulani ya kiungo kama katika suala hili la kidole kwa sababu ya pete iliyobana. Itabidi mtu huyo avue pete yake wakati wa kutawadha ili wudhuu wake uwe sahihi. Bila ya hivyo atakuwa hana Swalah. Na Allaah Anajua zaidi






Vitambulisho:




Nabeel Al Refaie - Quran Downloads